Ni kweli kuwa simu za Tecno kwa hapa Tanzania ni moja kati ya simu zinazotumiwa na watu wengi sana, kuliona hilo ndio maana leo nimeamua kukuletea list hii ya simu za tecno au simu 10 bora za tecno ambazo ni nzuri na bora sana kuwa nazo kwa mwaka huu 2020.
Vilevile kwenye list hii tutenda kuangalia bei za simu za tecno pamoja na upatikanaji wake hii ikiwa na maana mahali pakuzipata au kununua simu hizo hasa zilizopo kwenye list hii ya simu bora za tecno kwa mwaka huu 2020. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie list hii.
13. Tecno WX4 PRO
Simu ya Tecno WX4 PRO ni moja kati ya simu ambayo ni juu ya simu ya toleo la simu ya Tecno WX4, simu hii ni bora sana kwa wale wanaopenda simu za tecno za bei rahisi na simu hii inauwezo mzuri wa RAM pamoja na uwezo wa Mtandao wa mtandao wa 4G.
Sifa za Tecno WX4 PRO
- Uwezo wa Kioo – 5-inch Touch Screen Display, 720 x 1280 pixels (294ppi)
- Uwezo wa Processor – 1.25GHz quad-core CPU with a 2GB of RAM
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 (Nougat)
- Ukubwa wa Ndani – GB 16 unaweza kuongeza kwa memory kadi ya GB 32
- Uwezo wa Kamera – Kamera ya Nyuma Megapixel 8, Kamera ya Nyuma Megapixel 8, inayo flash kwenye kamera ya mbele na Nyuma.
- Uwezo wa Ulinzi – Inayo sehemu ya Fingerprint Sensor (Rear)
- Uwezo wa Network – 4G, 3G pamoja na 2G
- Uwezo wa Battery – Battery yenye uwezo wa 2800 mAh ambayo inatoka (Removable Battery) yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa siku moja ikichajiwa vizuri.
- Bei – TSH 350,000 – 250,000 Inategemea na Utakapo Nunua
- Inapo Patikana – Kwenye duka la Tecno kariakoo.
NUNUA WX4 (SIO PRO) KWA TSH 196,000
12. Tecno L9
Simu za tecno L zinajulikana sana kwa uwezo wake mkubwa wa kudumu na chaji na Tecno L9 nayo pia haiko mbali sana na uwezo wa simu hizi. Simu hii ya Tecno L9 inakuja na battery kubwa sana ya 4000mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji siku mbili endapo itachajiwa vizuri.
Sifa za Tecno L9
- Uwezo wa Kioo – 5.5 inches, 720 x 1280 pixels screen display, 267 pixels per inch (PPI)
- Uwezo wa Processor – 1.3GHz quad-core Cortex-A53 CPU, MediaTek MT6735M chipset pamoja na Mali-T720 GPU
- Uwezo wa RAM – 1GB of RAM
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 6.0 with HIOS V1.0
- Ukubwa wa Ndani – GB 16 yenye uwezo wa kusoma memory kadi hadi ya GB 128
- Uwezo wa Kamera – Kamera ya nyuma Megapixel 8, Kamera ya Mbele Megapixel 5
- Uwezo wa Network – 3G na 2G
- Uwezo wa Battery – 4000 mAh Li-ion yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa siku mbili ikichajiwa vizuri.
- Bei – Tsh 380,000 – 350,000 Inategemea na Utakapo Nunua
- Inapo Patikana – Duka la Tecno kariakoo
11. Tecno Camon C7
Simu ya Tecno camon C7 ni moja kati ya simu bora sana kuwa nayo hasa kwa wale ambao wanapenda kupiga picha maarufu kama selfie, simu hii inakuja na kamera kubwa ya mbele ya Megapixel 13 pamoja na aina mpya ya ulinzi wa Iris scanner Biometric Authentication ambao inafanya kazi pamoja na sehemu ya Fingerprint.
Sifa za Tecno Camon C7
- Ukubwa wa Kioo – 5-inch IPS Screen Display, 720 x 1280 pixels (400 ppi)
- Uwezo wa Processor – 1.3GHz quad-core with MediaTek CPU and 2GB of RAM
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 6.0 with HIOS V1.0
- Ukubwa wa Ndani – GB16 pamoja na uwezo wa kusoma memory kadi hadi ya GB 128
- Uwezo wa Kamera – Kamera ya Mbele Megapixel 13, Kamera ya Nyuma Megapixel 13.
- Uwezo wa Network – 3G/4G LTE
- Aina ya Ulinzi – Fingerprint Sensor (kwa nyuma) and Iris Scanner (kwa mbele)
- Uwezo wa Battery – Battery yenye ukubwa wa 2500 mAh Li-ion Battery yenye uwezo wa kudumu siku moja ikichajiwa vizuri.
- Bei – TSH 300,000 – 250,000 Inategemea na Utakapo Nunua
- Mahali inapo Pataikana – Duka la Tecno Kariakoo
10. Tecno L9 Plus
Ni wazi kila simu iliyo ingia kwenye list hii ina sababu ya kuwa hapa, pengine bei yake kuwa rahisi, pengine sifa bora zaidi pengine ni uwezo wa simu kwa upande wa battery. Sasa kama ulikuwa unatafuta simu bora yenye uwezo wa kudumu na chaji zaidi basi simu hii ya Tecno LPlus ni moja kati ya simu bora sana kwako. Simu hii ina battery yenye ukubwa wa 5000mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa zaidi ya masaa zaidi ya 72 ambayo ni sawa na siku tatu.
Sifa za Tecno L9 Plus
- Uwezo wa Kioo – 6.0-inch IPS Screen Display, 720 x 1280 pixels (244ppi)
- Uwezo wa Processor – 1.3GHz quad-core with MediaTek CPU and 2GB of RAM
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 with HiOS
- Ukubwa wa Ndani – 16GB Storage expandable up to 128GB
- Uwezo wa Kamera – Kamera ya nyuma Megapixel 13, Kamera 5MP Selfie Camera
- Uwezo wa Network – 3G Internet
- Aina ya Ulinzi – Fingerprint Sensor (Rear)
- Uwezo wa Battery – 5000 mAh Battery yenye teknolojia ya Fast Charging
- Bei – TSH 500,000 – 400,000 Inategemea na Utakapo Nunua
- Mahali inapo Patikana – Duka la Tecno Kariakoo
9. Tecno Camon C9 au Tecno Camon C9 Plus
Mpaka sasa bado simu ya Tecno camon C9 inaendelea kushikilia chati ya simu bora zenye uwezo mzuri sana wa kamera, simu hizi ambazo zina kamera yenye nguvu zaidi ni bora sana kwa wale wanaopenda kupata simu zenye uwezo mkubwa wa RAM pamoja na kamera.
Sifa za Tecno Camon C9
- Ukubwa wa Kioo – 5.5-inch IPS Screen Display, 1080 x 1920 pixels (400ppi)
- Uwezo wa Processor – 1.3GHz octa-core with MediaTek MT6753 CPU and 2GB/3GB of RAM
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 6.0. Marshmallow
- Ukubwa wa Ndani – 16GB Storage expandable up to 32GB
- Uwezo wa Kamera – 13MP Back Camera and 13MP Selfie Camera
- Uwezo wa Network – 4G LTE Data
- Aina ya Ulinzi – Iris Scanner (Front)
- Bei – 250,000 – 450,000 Inategemea na Utakapo Nunua
- Mahali inapo patikana – Duka la Tecno Kariakoo
8. Tecno Camon CX Air
Simu hii pia ya Tecno Camon CX Air nayo ni moja kati ya simu ambazo ni bora kwa wale wanaopenda kuwa na simu zenye uwezo mkubwa wa kamera, Mbali na kuwa na uwezo mkubwa sana wa kamera simu hii pia inapatika kwa bei nafuu sana.
Sifa za Tecno Camon CX Air
- Ukubwa wa Kioo – 5.5-inch IPS Screen display, 720 x 1280 pixels (267ppi)
- Uwezo wa Processor – 1.25GHz quad-core with MediaTek MT6737 CPU and 2GB of RAM
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 with HiOS 2.0
- Ukubwa wa Ndani – Ukubwa wa ndani GB 16 inayo weza kuongezwa kwa memory kadi hadi ya GB 128.
- Uwezo wa Kamera – Kamera ya Nyuma Megapixel 13 Kamera ya Mbele Megapixel 13
- Uwezo wa Internet – 4G LTE (up to 150Mbps)
- Aina ya Ulinzi – Fingerprint Sensor (Rear)
- Uwezo wa Battery – Ukubwa wa battery 3200 mAh yenye teknolojia ya Fast Charging
- Bei – 350,000 au 380,000 inategemea na mahali ulipo nunua.
- Mahali inapo patikana – Duka la Tecno lililopo Kariakoo Dar es Salaam. Mkuoani Wakala wa Tecno pamoja na Kwenye mtandao wa Jumia.
7. Tecno Camon CX Manchester City Edition
Kama wewe ni mpenzi wa simu zenye uwezo mzuri wa kupiga picha hasa za Selfie basi simu ya Tecno Camon CX ni simu bora sana kwako, Mbali na uwezo wake mkubwa kwenye upande wa kamera simu hii iko vizuri pia kwenye upande wa ulinzi wa fingerprint, sehemu yake ya fingerprnt inauwezo mkubwa sana wa kusoma alama zako za vidole kwa haraka zaidi pengine kuliko simu nyingine kwenye list hii.
Sifa za Tecno Camon CX
- Ukubwa wa Kioo – 5.5inch, PPI 404
- Uwezo wa Processor – Octa-Core Cortex A53,1.5GHz 4GB of RAM
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 with HiOS 2.0
- Ukubwa wa Ndani – Ina ukubwa wa ndani wa GB 16 unao weza kuongezwa kwa memory kadi ya GB 28
- Uwezo wa Kamera – Kamera ya Nyuma Megapixrl 16, Kamera ya Mbele Megapixel 16
- Uwezo wa Network – 4G LTE (up to 300Mbps)
- Aina ya Ulinzi – Fingerprint Sensor (Back)
- Uwezo wa Battery – Ina uwezo wa battery yenye ukubwa wa 3200 mAh pamoja na teknolojia ya Fast Charging
- Bei – TSH 650,000 – 550,000 Inategemea na Utakapo Nunua
- Mahali inapo patikana – Kwenye Duka la Tecno Kariakoo
6. Tecno Camon CM
Tecno Camon CM ni moja kati ya simu za kisasa sana kutoka kampuni ya Tecno, simu hii inakuja na muundo mpya na wakuvutia sana huku ikipendezeshwa na kioo cha Full Display ambacho kianuwezo wa kuonyesha rangi zaidi ya milioni 16. Kama unatafuta simu ya kisasa yenye muonekano mzuri basi Tecno Camon CM ni simu bora sana kwako.
Sifa za Tecno Camon CM
- Ukubwa wa Kioo – 5.65-inch yenye resolution ya 720 x 1440 pixels, Full Vision capacitive touchscreen
- Uwezo wa Network – 2G/3G/4G
- Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye FF pamoja na Ring-Flash (Quad-Flash)
- Kamera ya Mbele – Megapixel 13 yenye FF, pamoja na Dual-Flash
- Uwezo wa Processor – Quad-Core 1.3GHz yenye uwezo wa 64-bit MEDIATEK MTK6737H
- Uwezo wa GPU – Mali-T720
- Ukubwa wa Ndani – GB 16 inayoweza kuongezeka kwa memory card hadi 128GB
- Ukubwa wa RAM – GB2
- Mfumo wa uendeshaji – Android 7.0 Nougat yenye HiOS 2.0 User Interface
- Uwezo wa Bluetooth – V4.1
- Uwezo wa Battery – battery ya Li-Polymer yenye ukubwa wa 3050mAh, pamoja na teknolojia ya Fast Charging.
- Bei – TSH 500,000 – 450,000 Inategemea na Utakapo Nunua
- Inapo Patikana – Kwenye Duka la Tecno Mlimani City, Duka la Tecno Kariakoo
5. Tecno Phantom 6 au Phantom 6 Plus
Tecno Phantom 6 imekuwa ni simu bora sana kwa muda mrefu sasa tangu kutoka kwake mpaka sasa hii ni moja kati ya simu za kipekee sana kutoka kwa kampuni ya Tecno. simu hii mbali na kuwa na sifa bora sana, simu hii pia ina uwezo mkubwa wa RAM uwezo mkubwa wa ukubwa wa ndani na mengine mengi. Kama unatafuta simu ya kudumu nayo kwa muda mrefu basi Tecno Phantom 6 au 6 Plus ni simunzuri sana kwaajili yako.
Sifa za Tecno Phantom 6
- Uwezo wa Network – 2G, 3G, 4G LTE.
- Uwezo wa Kioo – Display: 6.0-inch Amoled with 1920 x 1080 Pixels screen resolution and 420 PPI.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 6.0 Marshmallow.
- Uwezo wa Processor – 2.0GHz Helio X20 Octa-core Mediatek Chipset.
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 Inayoweza kuongezwa kwa memory kadi ya GB 128
- Uwezo wa Kamera – Kamera ya Nyuma Megapix 13MP AF & 5MP Sony IMX Dual Back Camera with autofocus and dual LED flash. Kamera ya Mbele Megapixel 5
- Uwezo wa Battery – Non removable 2700 mAh.
- Aina ya Ulinzi – Iris Scanner 2.0.
- Bei – Phantom 6 Plus TSH 800,000 – 750,000 Inategemea na Utakapo Nunua
- Mahali Pakununua – Duka la Tecno Kariakoo, Duka la Tecno Mlimani City
4. Tecno Phantom 8
Tecno Phantom 8 ni moja kati ya simu za kisasa sana sana, simu hii inauwezao mkubwa sana pamoja na sifa ambazo zinafanya simu hii kuwa ya kipekee sana kwenye list hii, simu hii mbali na kuwa bora kwenye upande wa kamera lakini pia simu hii ni bora sana kwenye upande wa sifa. Hivyo basi kama unataka kuwa wa kisasa na kutumia simu yenye uwezo mkubwa kwenye kila panda basi simu hii ya Tecno Phantom 8 ni simu bora sana kwako.
Sifa za Tecno Phantom 8
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.7 huku ikiwa na resolution ya 1920 x 1080, pamoja na kioo chenye teknolojia ya IPS.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat with HiOS 3.0.
- Uwezo wa Processor – Octa core 2.6 GHz huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya MediaTek Helio P25.
- Uwezo wa RAM – GB 6.
- Ukubwa wa Ndani – GB 64.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G.
- Kamera ya Mbele – Megapixel 20, Huku ikiwa na Dual-LED flash.
- Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine yenye Megapixel 13 zote zikiwa na teknolojia ya Telephoto for 2x zoom.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint iliyoko kwa nyuma.
- Uwezo wa Battery – 3500 mAh huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya Li-Io
- Bei – TSH 900,000 – 800,000 Inategemea na Utakapo Nunua
- Mahali Inapo Patikana – Duka la Mlimani City, Duka la Tecno Kariakoo.
Update Tarehe 26-04-2018
Makala hii imeongezewa simu nyingine za tecno ambazo zimezinduliwa hivi karibuni, simu hizi zilizo ongezwa pia ni bora na zinaweza kupatikana hapa Tanzania na unaweza kuona bei za simu hizo chini ya sifa za simu hizi.
3. Tecno Camon X na Tecno Camon X Pro
Hii ni simu mpya kwa sasa kutoka Tecno simu hii inasifika kwa ubora wake wa kupiga picha nzuri sana, simu hizi zinakuja na machaguo mawili ya Tecno Camon X pamoja na Tecno Camon X Pro. Simu ya Tecno Camon X Pro yenyewe ina kamera kubwa zaidi, sifa nyingine za simu hiyo ni kama zifuatazo.
Sifa za Tecno Camon X
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.00 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 1080 x 2160 pixels, 18:9 ratio (~269 ppi density)
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0GHz MediaTek Helio P23
- Uwezo wa GPU – Mali-T720
- Ukubwa wa Ndani – GB 16 kwa Tecno Camon X na GB 64 kwa Tecno Camon X Pro zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 128.
- Ukubwa wa RAM – GB 3 kwa Tecno Camon X na GB 4 kwa Tecno Camon X Pro
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 kwa Tecno Camon X Pro na Megapixel 20 kwa Tecno Camon X zote zikiwa na Ring flash
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 ikiwa na Dual-flash
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3750 mAh battery
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, A2DP, LE
pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB 2.0 - Rangi – Inakuja kwa rangi ya Midnight Black
- Mengineyo – Inayo Line Mbili za Dual SIM
- Ulinzi – Fingerprint (iko nyuma), Face Unlock (kufungua simu kwa uso)
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- BEI – Tecno Camon X Tsh 550,000 hadi Tsh 470,000 na Tecno Camon X Pro Tsh 700,000 hadi Tsh 600,000.
- Mahali Inapo Patikana – Maduka ya Tecno, Kupita Jumia
2. Tecno Spark 2
Tecno Spark 2 ni simu nyingine nzuri ya TECNO ya kununua kwa mwaka huu 2020, simu hii ni maalum kwa wale wanaotaka simu za bei nafuu na zenye sifa za kawaida. Tecno Spark 2 inakuja na mfumo wa Android Go ambao mfumo huu ni maalum kwa simu zenye RAM ya GB 1, sifa nyingine za Tecno Spark 2 ni kama zifuatazo.
Sifa za Tecno Spark 2
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.00 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 720 x 1440 pixels, 18:9 ratio (~274 ppi density)
- Mfumo wa Uendeshaji – Android GO 8.1 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – quad-core 1.3 GHz ARM Cortex-A7 MediaTek Mt6580 chipset
- Uwezo wa GPU – Mali-400MP2
- Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 128.
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 MP, f/2.4 dual-LED flash.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 autofocus, quad-LED flash
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, A2DP, LE
pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB 2.0 - Rangi – Inakuja kwa rangi za Champagne Gold, Choral Blue, Metal Silver and Phantom Black
- Mengineyo – Inayo Line Mbili za Dual SIM
- Ulinzi – Fingerprint (iko nyuma), Face Unlock (kufungua simu kwa uso)
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Bei – Tsh 300,000 – 350,000
1. Tecno Camon 11
Tecno Camon 11 ni simu nyingine nzuri sana kutoka kampuni ya Tecno, Kama wewe ni mpenzi wa simu yenye kamera nzuri na ya kisasa basi Camon 11 au Camon 11 Pro ni simu nzuri sana kuwa nayo kwa mwaka huu. Simu hii pia inakuja na battery yenye uwezo wa kudumu chaji zaidi kulingana na matumizi pengine kuliko simu nyingine kwenye list hii.
Sifa za Tecno Camon 11
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~269 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) na HiOS 4.1
- Uwezo wa Processor – Octa-Core 2.0GHz.
- Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek Helio P22 Chipset.
- Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
- Ukubwa wa RAM – GB 3.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye teknolojia ya AI pamoja na LED Flash
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine inakuja na Megapixel 2 zenye AI, Autofocus na Flash ya Dual-LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3750 mAh battery.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS. USB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Red, Black na Blue
- Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM,), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Light Sensor, Compass, Proximity Sensor, Face ID Sensor na Fingerprint.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), na Ulinzi wa kutambua uso (Face ID).
Tecno Spark 3
Tecno Spark 3 na Spark 3 Pro ni simu mpya kabisa kutoka kampuni ya Tecno kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda simu za tecno zenye sifa za kawaida pamoja na uwezo mzuri wa kamera basi simu hii ni simu nzuri sana kwako. Tecno Spark 3 Pro inakuja na uwezo mkubwa zaidi kuliko Spark 3, lakini zote zinafanana kwa sura. Zifuatazo ni baadhi ya sifa za Tecno Spark 3.
Sifa za Tecno Spark 3
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Quad-core CPU (4×1.3, GHz Cortex-A53).
- Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek MT6761
- Uwezo wa GPU – Mali G71.
- Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
- Ukubwa wa RAM – GB 2
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.9, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye f/2.2. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3500 mAh.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ocean Blue na Charcoal Black.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G na 3G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
TECNO Phantom 9
Phantom 9 ni moja kati ya simu bora sana kwa mwaka huu 2020, kama wewe ni mpenzi wa simu bora basi Phantom 9 ni simu bora sana kwako. Simu hii inakuja na kamera bora na pia inakuja na kioo kizuri cha AMOLED ambacho kinafanya simu hii kuonyesha rangi bora sana. Hizi hapa ni baadhi ya sifa za TECNO Phantom 9.
Sifa za TECNO Phantom 9
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.35 GHz Cortex-A73 & 4×2.0 GHz Cortex-A53)
- Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6765 Helio P35 (12 nm).
- Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
- Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezwa na memory card ya microSD ya hadi GB 500.
- Ukubwa wa RAM – GB 6.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16, PDAF na kamera nyingine ikiwa na Megapixel 8 na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3500 mAh battery.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, 4.2, A2DP, HD, LE
na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go. - Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Aurora Blue.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).
Na hizo ndio simu bora za Tecno ambazo unaweza ukanunua kwa mwaka huu 2020, List hii haina maana kuwa hizi ndio simu nzuri zaidi kutoka kampuni ya Tecno HAPANA Bali list hii ni baadhi ya simu zenye ubora kwa namna moja ama nyingine kutokana na vitu mbalimbali kama ubora wa kamera, ubora wa battery, ubora wa muundo, pamoja na ubora wa bei. Na kuchangiwa na mambo mengine mengi tuliyo yangalia kabla ya kuleta list hii.
Bado zipo simu nyingi sana nzuri kutoka kampuni ya Tecno na ningependa kusikia kutoka kwako, je kwa upande wako wewe ni simu gani 10 bora kutoka kampuni ya Tecno na ni kwa sababu gani..? tuambie kwenye maoni hapo chini na tutahakikisha tunafanyia uchunguzi na kuingiza simu hizo kwenye list nyingine ya simu bora za kununua kutoka Tecno. Kumbuka, unaweza kusoma hapa list ya ujumla ya simu nyingine 10 bora za kununua kwa sasa.
Nawashukuru kutufahamisha kila mara simu nzuri na sifa zake big up sana.
Karibu sana
Aisee big up sana this is the best blog i see so far… Keep up
Asante sana Mdosho
Nimependa taarifa hii Ongereni kwa yote.
Karibu sana
Nahitaji k7+ au w5 used kwa bei nafuu zinapatkana
Gasper Abull
inasaidia sana mtu ukienda dukani unajua nini unataka na bei da asanteni sana
Karibu
Mpo vizuri ila nahitaji tecno w5 ni bei gani?
Asanteni sana tecno Tz ila vitu kwenye box havi timi au madukani wana vitoa
Inapendeza sana
Maoni*TSH1500,00 NITAPATA
Maoni*9
Nataka kujua being ya tecno k9 plus being yake
Maoni*safi sana kwa habari njema
je naweza kupata simu ya tecno wx3 kwa bei gani
Jee Tecno Y4 inafaa?
Tecno l9 plus naweza kuipata kwa bei gan?
mko juuuuu
Mjitahidi taarifa ziwe sahihi, nimewahi tumia tecno l9 plus, ram ni 2gb sio kama mlivyosema
Asante muchuno Tayari tumesha rekebisha
Naitaji simu ya tecno C8 yabei nafuu
Naitaji simu aina ya tecno C8 yabei nafuu
Thanks for this Wonderful Blog. I’m convinced to download your App.
Big Up Sana
Nahitaji kioo cha tecno camon x air ni sh ngapi?
Hatujafahamu bei ya vifaa hivyo vya simu unaweza kutemebela maduka mbalimbali ya vifaa vya tecno kariakoo au maduka mengine kama uko nje ya nchi.
Tecno pouvior 2 inauzwaje bei ya promotion
Iko poa sana
Aaaaa uko mzima?
Nimepende huduma zenu ivi naweza kubadilisha mwandiko kwenye simu ya Tecno spark 2
Ndio
Sisi wa mikoani inawezekana kutumiwa
Nahitaji camon x pro ntaipata kwa TSH ngapo
Tecno Spark 2 inakubali Memory card mpaka ya ukubwa wa GB 128? Vile vile ina 4G LTE?
Ndio
Pls bei ya tecno w5 lite
Maoni*nahitaji tecno c 9 plus
Simu yenye uwezo mkubwa zaidi ni ipi?
Unaweza kurudia swali lako tafadhali.
Tecno phantom 8
nahitaji kuiyona tecno fire
Naomba kuuliza,,,Tecno toleo jipya zilotoka hivi karibuni ni lipi?? tecno gani???
Tecno Phantom 9 au 10
DA NIMEWAKUBALI SAANA HASA KWA SS WATU WA CHINI KWA HIZO BEI NA UBORA WA SIMU ZENU NAITWA RAMA MWALENI ARUSHA TZ
Mbona amjaweka picha ya spark2
NATUMIA K7..ILA INASUMBUA SANA SOMETIMES INAWEZA TOUCH IKAZNGUA WIKI NZIMA ISIFANYE KAZ NA HAIKAI NA CHAJI….HAYA MATATIZO YANAWEZA TATULIKA….?????
Aksantenui kwa kazi yenu wengi tunazujua simu hapa. advice kwa sababu wenngi wanapenda simu zaa smartiphone but ywezo wao ni wachini basi muwe mnaposti na smatiphone za bei za chini zaidi na za gar zaid. Kwa mfano simu za bei gar zaid ni hizi hapa….. na bei za bei za chini zaidi ni hizi hapa…… but hongereni kazi ni nzuri…..
Maoni*nimepnda techno phantom 6 bei sh ngapi wakuu?
Big Up Ingawa Natumia Tecno P3
Inapendeza sana
dah hili toleo lenu jipya nmelipenda sana dah big up ila nmeipenda sana tecno como CM
maelezo ya tecno n8 kama ulivyofanya kwa simu hizo nyingine
je kama naitaji sim kwenu lakini sina hela ya kutosha je naweza kuwekeza kidogo kidogo?
Asant sana kwa taarifa, coz zinaturahisishia kujua aina ya simu ya bei yke hata napotaka kununua ,But Nina Techno K7,honestly inaboa hatari, ina stuck kuliko kawaida. We love u, so tupeni bidhaa rafiki
Mimi natumia Tecno spark 2 ila 4g mbn haikubaliki na ni toleo la mapema zaidi
safi
sasa simu hizo mpaka k koo na Mimi wa mkoani inakuaje!
Hata mkoani unazipata
Maoni*
Nahitaji kuipata wx4 pro
Kila nikiulizia madukan naambiwa toleo Hilo halipo tena, mnanisaidieje ili niipata?
Nahitaji kuipata wx4 pro Kila nikiulizia madukan I naambiwa toleo Hilo halipo tena, mnanisaidieje niweze kuipata?
Maoni*Nigependa Kufahamu Kati Ya Hizo Ni Zipi Ziko Na Video Call
Simu zote zenye camera ziko na video call ndugu
mpo vizur sana tecno
Maoni*asanten sana
Bado kiukweli cm za tecno battery AM zipo very very low