Samsung ni moja kati ya kampuni za utengenezaji wa simu yenye simu nyingi pengine kuliko kampuni nyingine za utengenezaji wa simu hasa za Android. Kutokana na hayo nimeona kuna uhitaji wa kuja na list hii ya simu bora za Samsung ambayo itakuwezesha kujua simu bora za kununua ndani ya mwaka huu 2019. Lakini kabla ya kuanza labda niweke wazi kuwa, kuna simu nyingi sana za Samsung hivyo tumejitahidi kufanya uchunguzi wa hali ya juu na kuja na list hii lakini pia inawezekana kuna baadhi ya simu hazipo kwenye list hii hivyo unaweza kuchangia kupitia sehemu ya maoni kama utaona kuna simu imesahaulika.
TABLE OF CONTENTS
- 1 1. Samsung Galaxy S9 na S9 Plus
- 2 2. Samsung Galaxy Note 8
- 3 3. Samsung Galaxy S8 na S8 Plus
- 4 4. Samsung Galaxy S7 na S7 Edge
- 5 5. Samsung Galaxy A8 na A8 Plus (2018)
- 6 6. Samsung Galaxy A7 (2017)
- 7 7. Samsung Galaxy A5 (2017)
- 8 8. Samsung Galaxy C9 Pro
- 9 9. Samsung Galaxy C7 Pro (2017)
- 10 10. Samsung Galaxy J7 Max (2018)
- 11 11. Samsung Galaxy A7 (2018)
- 12 12. Samsung Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus
- 13 13. Samsung Galaxy A80
- 14 14. Samsung Galaxy A10
- 15 15. Samsung Galaxy A20
- 16 16. Samsung Galaxy A30
- 17 17. Samsung Galaxy A50
1. Samsung Galaxy S9 na S9 Plus
Najua hapa sina haja ya kusema sana, Simu za Galaxy S9 ni Simu nzuri sana kununua kwa sasa, simu hizi zinakuja na sifa na uwezo mzuri sana hasa kwa wale watu wanao pendelea picha au kamera yenye uwezo mkubwa. Simu hizi kwa sasa zinapatikana hapa Tanzania na unaweza kuzipata kupitia maduka mbalimbali pamoja na masoko ya mtandao. Bei ya S9 ina anzia Tsh 2,300,000 hadi Tsh 2,500,000 Simu ya Galaxy S9 Plus ina anzia Tsh 3,000,000 hadi Tsh 2,800,000.
- Dimensions: 158.1 x 73.8 x 8.5mm
- OS: Android 8
- Screen size: 6.2-inch
- Resolution: 1440 x 2960
- CPU: Octa-core (4×2.7 GHz Mongoose M3 & 4×1.8 GHz Cortex-A55)
- RAM: 6GB
- Storage: 64GB/128GB
- Battery: 3,500mAh
- Rear camera: Dual 12MP
- Front camera: 8MP
2. Samsung Galaxy Note 8
Pamoja na kwamba simu hii ilikuwa na majanga kidogo, lakini hii ni moja kati ya simu ambazo ni nzuri sana na sifa zake ni kama za S9 lakini ni tofauti kidogo kwenye upande wa kamera, Simu hii inasifa nzuri sana na uwezo wa kipekee na kama ulikuwa unatafuta simu bora ya kununua mwaka huu badala ya S9 basi hii pia ni simu nzuri sana ya kuwa nayo. Simu hii unaweza kuipata kwa Tsh 2,500,000 hadi Tsh 3,000,000.
- Dimensions: 162.5 x 74.8 x 8.6mm
- OS: Android 8
- Screen size: 6.3-inch
- Resolution: 1440 x 2630
- CPU: Octa-core (4×2.3 GHz Mongoose M2 & 4×1.7 GHz Cortex-A53)
- RAM: 6GB
- Storage: 64GB/128GB/256GB
- Battery: 3,300mAh
- Rear camera: Dual 12MP
- Front camera: 8MP
3. Samsung Galaxy S8 na S8 Plus
Hapa pia sina haja ya kusema maneno mengi sana, wote tunaijua simu ya Samsung Galaxy S8 na S8 Plus. Simu hii pia ni moja kati ya simu ya Samsung ambayo ni bora sana kuwa nayo kwani simu hii ina uwezo mkubwa sana pamoja na sifa za kipekee. Unaweza kuipta Samsung Galaxy S8 kwa Tsh 2,000,000 hadi Tsh 1,800,000. Kwa upande wa Galaxy S8 Plus utaipata kwa Tsh 2,500,000 hadi Tsh 2,050,000.
- Dimensions: 148.9 x 68.1 x 8mm
- OS: Android 8
- Screen size: 5.8-inch
- Resolution: 1440 x 2960
- CPU: Octa-core (4×2.3 GHz Mongoose M2 & 4×1.7 GHz Cortex-A53)
- RAM: 4GB
- Storage: 64GB
- Battery: 3000mAh
- Rear camera: 12MP
- Front camera: 8MP
4. Samsung Galaxy S7 na S7 Edge
Pamoja na kwamba imepita miaka kadhaa, lakini ukweli bado simu hii iko kwenye chat sanaa. Simu hii ni moja kati ya simu nyingine ya Samsung bora sana kuwa nayo, simu hii inauwezo wa kipekee na inasemekana mwaka huu simu hii pia inategemewa kupata toleo jipya la Android Oreo 8.0. Unaweza kupata S7 kuanzia Tsh 800,000 hadi Tsh 650,000 na S7 Edge unaweza kuipata kwa Tsh 900,000 hadi Tsh 750,000.
- Dimensions: 142.4 x 69.6 x 7.9mm
- OS: Android 7 – Android 8
- Screen size: 5.1-inch
- Resolution: 1440 x 2560
- CPU: Octa-core (4×2.3 GHz Mongoose & 4×1.6 GHz Cortex-A53)
- RAM: 4GB
- Storage: 32GB
- Battery: 3,000mAh
- Rear camera: 12MP
- Front camera: 5MP
5. Samsung Galaxy A8 na A8 Plus (2018)
Galaxy A8 (2018) ni moja kati ya simu zenye muundo mzuri sana, mbali ya kuwa na muundo mzuri simu hii ina sifa nzuri sana na makini. Kwa wale wanaopenda simu za samsung basi ni vyema ufahamu simu hii kwani ni moja kati ya simu bora sana yaani sana. Unaweza kuipta A8 kuanzia Tsh 1,200,000 hadi Tsh 750,000 na unaweza kupata A8 Plus kwa Tsh 1,500,000 hadi Tsh 900,000.
- Dimensions: 149.2 x 70.6 x 8.4 mm (5.87 x 2.78 x 0.33 in)
- OS: Android 7.1.1 (Nougat)
- Screen size: 5.6-inch
- Resolution: 1080 x 2220 pixels
- CPU: Octa-core (2×2.2 GHz Cortex-A73 & 6×1.6 GHz Cortex-A53)
- RAM: 4GB
- Storage: 32GB/64GB
- Battery: 3,000mAh
- Rear camera: 16MP
- Front camera: Dual: 16 MP
6. Samsung Galaxy A7 (2017)
Samsung Galaxy A7 (2017) ni simu nyingine kutoka kampuni ya Samsung, Japokuwa simu hii ni ya mwaka mmoja ulipita lakini ukweli simu hii ni nzuri sana kwa sifa pamoja na muonekano. Kama wewe ni mpenzi wa simu za Samsung basi hakikisha simu hii inakuwa kwenye list ya simu kama unafikiria kwenda kutafuta simu nzuri ya kununua. Unaweza kuipata simu hii kuanzia Tsh 1,200,000 hadi Tsh 600,000.
- Dimensions: 156.8 x 77.6 x 7.9 mm (6.17 x 3.06 x 0.31 in)
- OS: Android 8.0 (Oreo)
- Screen size: 5.7 -inch
- Resolution: 1080 x 1920 pixels
- CPU: Octa-core 1.9 GHz Cortex-A53
- RAM: 3GB
- Storage: 32GB
- Battery: 3,600mAh
- Rear camera: 16MP
- Front camera: 16 MP
7. Samsung Galaxy A5 (2017)
Galaxy A5 2017 ni simu nyingine kwenye mfululizo wa simu za A Series, Simu hii ni nzuri sana na ukweli inauwezo mkubwa sana. Mbali na uwezo na Uzuri wa simu hii simu hii ni bora kwa wale wanapenda simu ndogo ambazo zinashikika mkononi. Unaweza kupata simu hii kwa Tsh 800,000 hadi Tsh 600,000.
- Dimensions: 146.1 x 71.4 x 7.9 mm (5.75 x 2.81 x 0.31 in)
- OS: Android 8.0 (Oreo)
- Screen size: 5.2 -inch
- Resolution: 1080 x 1920 pixels
- CPU: Octa-core 1.9 GHz Cortex-A53
- RAM: 3GB
- Storage: 32GB/64GB
- Battery: 3,000mAh
- Rear camera: 16MP
- Front camera: 16 MP
8. Samsung Galaxy C9 Pro
C9 Pro ni simu nyingine kutoka Samsung ambayo ni bora na yenye sifa nzuri yaani kuliko baadhi ya simu za Samsung za Toleo la Galaxy S. Mbali ya kuwa na sifa nzuri simu hii ni ngumu sana na kiukweli inadumu sana. Kwa mujibu wa maoni mbalimbali simu hii ni bora zaidi kuliko hata Galaxy S8. Unaweza kuipata kwa Tsh 1,300,000 hadi Tsh 800,000.
- Dimensions: 162.9 x 80.7 x 6.9 mm (6.41 x 3.18 x 0.27 in)
- OS: Android 7.1.1 (Nougat)
- Screen size: 6.0 -inch
- Resolution: 1080 x 2220 pixels
- CPU: Octa-core (4×1.95 GHz Cortex-A72 & 4×1.4 GHz Cortex-A53)
- RAM: 6GB
- Storage: 32GB/64GB
- Battery: 4,000mAh
- Rear camera: 16MP
- Front camera: 16 MP
9. Samsung Galaxy C7 Pro (2017)
Kama ilivyo C9 Pro, toleo la Samsung Galaxy C7 Pro pia ni toleo bora la simu za samsung, simu hii inatamba sana kwa kuwa na ubora wa hali ya juu. Mbali na sifa zake simu hii unaweza kudumu nayo kwa muda mrefu kutokana na ugumu wake. Unaweza kuipata C7 Pro kwa Tsh 1,200,000 hadi Tsh 900,000.
- Dimensions: 156.5 x 77.2 x 7 mm (6.16 x 3.04 x 0.28 in)
- OS: Android 7.0 (Nougat)
- Screen size: 5.7 -inch
- Resolution: 1080 x 1920 pixels
- CPU: Octa-core 2.2 GHz Cortex-A53
- RAM: 4GB
- Storage: 64GB
- Battery: 3,300mAh
- Rear camera: 16 MP
- Front camera: 16 MP
10. Samsung Galaxy J7 Max (2018)
Samsung Galaxy J7 Max ni simu nyingine kutoka Samsung ambayo ukweli ni simu bora sana, simu hii inauwezo mzuri sana pamoja na muonekano mzuri. Japokuwa simu hii ni ya mwaka jana lakini naweza kukwambia kuwa bado simu hii ni simu bora sana. Unaweza kuipata simu hii kwa Tsh 700,000 hadi Tsh 650,000.
- Dimensions: 156.7 x 78.8 x 8.1 mm (6.17 x 3.10 x 0.32 in)
- OS: Android 7.0 (Nougat)
- Screen size: 5.7 -inch
- Resolution: 1080 x 1920 pixels
- CPU: Octa-core (4×2.35 GHz Cortex-A53 & 4×1.65 GHz Cortex-A53)
- RAM: 4GB
- Storage: 32GB
- Battery: 3,300mAh
- Rear camera: 13 MP
- Front camera: 13 MP
11. Samsung Galaxy A7 (2018)
Kama unataka kwenda na wakati na kama wewe ni mmoja wa watu wanao pendelea picha basi Galaxy A7 (2018) ni simu bora sana kwako. Mbali ya kuwa na sifa nzuri sana simu hii ni moja kati ya simu za kwanza kabisa kutoka samsung zenye uwezo wa kamera tatu kwa nyuma. Unaweza kupata simu hii kwa makadirio ya Tsh 950,000 hadi 1,000,000 kwenye maduka mbalimbali ya Samsung hapa Tanzania. Zifuatazo ni baadhi tu ya sifa za Samsung Galaxy A7 (2018).
- Dimensions: 159.8 x 76.8 x 7.5 mm (6.29 x 3.02 x 0.30 in)
- OS: Android 8.0 (Oreo)
- Screen size: 6.0 -inch
- Resolution: 1080 x 2220 pixels
- CPU: Octa-core (2×2.2 GHz Cortex-A73 & 6×1.6 GHz Cortex-A53)
- RAM: 4GB/6GB
- Storage: 64GB/128GB
- Battery: 3,300mAh
- Rear camera: 24 MP, 8 MP, 5 MP.
- Front camera: 24 MP
12. Samsung Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus
Samsung Galaxy S10 na S10 Plus ni moja kati ya simu bora sana hadi sasa kutoka Samsung, Simu hizi zinakuja na uwezo mkubwa zaidi huku ikikupa uwezo zaidi kwenye kamera pamoja na ukubwa wa ndani. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda simu zenye uwezo mkubwa, au simu zenye sifa bora basi Galaxy S10 na S10 Plus ni simu nzuri sana kwaajili yako. Kwa sasa simu hizi zinatapatikana Tanzania (mpaka leo 27-01-2019 zinapatikana kwa pre-order) na unaweza kupata Galaxy S10 kwa Tsh 2,435,000 wakati Galaxy S10 Plus inapatikana kwa Tsh 2,715,000. Bei zote hizo zimejumuishwa na kodi.
- Dimensions: 157.6 x 74.1 x 7.8 mm (6.20 x 2.92 x 0.31 in)
- OS: Android 9.0 (Pie); One UI
- Screen size: 6.4 -inch
- Resolution: 1440 x 3040 pixels
- CPU: Octa-core (2×2.73 GHz Mongoose M4 & 2×2.31 GHz Cortex-A75 & 4×1.95 GHz Cortex-A55) – EMEA
- RAM: 12GB/8GB
- Storage: 128 GB / 512 GB / 1 TB
- Battery: 4100 mAh battery
- Rear camera: 12 MP, 12 MP, 16 MP.
- Front camera: 10 MP / 8MP
13. Samsung Galaxy A80
Galaxy A80 ni moja kati ya simu bora sana ya kuwa nayo kwa mwaka 2019, simu hii ni bora kwenye kila sekta na pengine naweza kukwambia simu hii ni bora kuliko hata Galaxy S10 au S10 Plus ambazo zimetoka mwaka huu 2019. Simu hizi zinapatikana kwa kati ya Tsh milioni 1.6 au pungufu.
- Dimensions: 165.2 x 76.5 x 9.3 mm (6.50 x 3.01 x 0.37 in)
- OS: Android 9.0 (Pie); One UI
- Screen size: 6.7 -inch
- Resolution: 1080 x 2400 pixels
- CPU: Octa-core (2×2.2 GHz Kryo 470 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 470 Silver)
- RAM: 8GB
- Storage: 128 GB
- Battery: 3700 mAh battery
- Rear camera: 48 MP, 8 MP, TOF Camera.
- Front camera: 48 MP, 8 MP, TOF Camera.
14. Samsung Galaxy A10
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanahitaji simu ya bei rahisi ya Samsung yenye kukidhi haja ya matumizi yako basi Galaxy A10 ni simu bora sana kwako. Mbali ya kuwa simu hii ni ya bei nafuu, pia vilevile inakuja na sifa nzuri kwa simu za bei hii. Kitu kikubwa kwenye simu hii ni pamoja na battery ambayo inaweza kudumu na chaji kwa muda wa siku moja nzima kulingana na matumizi yako.
- Dimensions: 155.6 x 75.6 x 7.9 mm (6.13 x 2.98 x 0.31 in)
- Resolution: 1080 x 2400 pixels
- CPU: Octa-core 1.6 GHz
- RAM: 3 GB
- Storage: 32 GB
- Display: IPS LCD, 6.2 inches
- Rear Camera: 13 MP
- Front Camera: 5 MP
- OS: Android 9.0 (Pie)
- Battery: 3500 mAh battery
15. Samsung Galaxy A20
Kama unatafuta simu ya Samsung yenye uwezo mzuri pamoja na sifa bora basi Galaxy A20 ni simu nyingine nzuri ya kununua kutoka kampuni ya Samsung, simu hii inakuja na uwezo mzuri wa battery na pia inakuja na kamera bora ambazo zinaweza kupiga picha vizuri sana, kama wewe ni mpenzi wa picha basi hakikia simu hii inakufaa sana.
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (2×1.6 GHz & 6×1.35 GHz).
- Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 7884 Octa (14 nm).
- Uwezo wa GPU – Mali-G71.
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – GB 3.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.9, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ocean Blue na Charcoal Black.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
16. Samsung Galaxy A30
Galaxy A30 ni simu nyingine nzuri ya Samsung ambayo unaweza kuipata kwa sasa hapa nchini Tanzania, simu hii inakuja na kioo kikubwa na inakuja na uwezo mzuri wa kamera pamoja na uwezo mkubwa wa kudumu na chaji. Mbali na hayo simu hii inakuja na mfumo wa kisasa wa Android 9 mfumo ambao unaweza kuongezewa na mfumo mpya wa Android 10
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, pamoja na uwiano wa 19.5:9 ratio (~403 ppi density.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz Cortex-A73 & 6×1.6 GHz Cortex-A53).
- Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 7885 Octa (14 nm).
- Uwezo wa GPU – Mali-G71.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 64 na nyingine inayo GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 3.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.7, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ocean Blue na Charcoal Black.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
17. Samsung Galaxy A50
Simu nyingine bora ya Samsung ya kuwa nayo kwa mwaka huu 2020 ni simu ya Galaxy A50, simu hii ni bora sana kuanzia kioo chake hadi battery. Simu hii inakuja na kamera bora ya Selfie ambayo inakuja na uwezo wa kuchukua video bora na picha zenye rangi angavu. Mbali na hayo simu hii inakuja na uwezo mkubwa wa RAM hivyo kama wewe ni mtu wa kutumia programu nyingi kwa wakati mmoja basi simu hii ni nzuri sana kwako.
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, pamoja na uwiano wa 19.5:9 ratio (~403 ppi density.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz Cortex-A73 & 6×1.6 GHz Cortex-A53).
- Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9610 Octa.
- Uwezo wa GPU – Bado Haijajulikana.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 128 na nyingine inayo GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na GB 4.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 25.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 25 yenye f/1.7, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, (ultrawide), na kamera ya tatu ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ocean Blue na Charcoal Black.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
Na hizo ndio simu za Samsung ambazo ni bora na ambazo unaweza kununua kwa sasa kupitia maduka mbalimbali yanayo uza simu za Samsung hapa Tanzania na Afrika Mashariki. Kama nilivyo sema hapo awali, list hii haina simu zote za Samsung hivyo unaweza kutuambia kwenye maoni kama kuna simu tuliyo isahau na sisi tutaweza kuongeza kwenye list hii moja kwa moja.
Nawakubali sanaaa
Karibu sana
nawakubari sana mko vizuri
Karibu sana, Ayubu
Kwa nn sim ya s9 na s8 being zao zinalingana na zko tafaut katika matumiz hebu naomba ufafanuz kidogo kuhusu ila namba 0778998120 au 0623600187
Mimi naitaji simu nzuri ya Samsung nichagulieni kati ya simu hizi zifuatazo Samsung A 5 ya mwaka 2017 na Samsung A 7 ya mwaka 2018. Pia niorodheshee bei za simu nilizozitaja, Namba yangu 0738744013, 0656974269 E mail daudiopiyo16@gmail.com
Maoni*A3 ni sh ngap
nawapongeza sana .kutokupoteza .nembo ya SAMSUNG .kwa juu ya kioo. sio nyuma ya kioo.
sio mpaka mtu aniulize ^*. eti simu gani.
inatakiwa yeye ndo usikie akisema
%+( SAMSUNG GALAXY )+%
mm sinaaa maoni ila nina swali limalosemaaaa kuwa kunatofautii gan kwenye hii simu ya A7 maama bei zake kuna ya 1200000 na 600000
Toeni na list ya Samsung zenye bei nafuu
J5 pro bei gani?
Sim zenu nazipenda ila bei zenu kubwa uwezo wa kuzinunua sina mnanisaidiaje kwa hilo ili na mimi nipate
Kilo cha s7 edge kimeharibika kinapatikana kwa being gan
Kioo cha samsung A10s kinauzwa sh ngapi dukani??
C5 pro inakua bei gani?
C5 pro bei gani?
Samsung galaxy j 6 sijaiona hapo bei yake
naomba namba zanu ofisini
Mimi natumia sumsung galaxy note8 ila nashndwa kuweka finger print security hivo nisahdie
Hakika Mko vizuri mno tena mno
Maoni*
mnapatikana wapi ?
wekeni namba za simu
Maoni*ninzur.san nimeipenda lakin vp kuhusu note3 beiyake kwamwaka huu ikoje
Na hitaji sumsung galaxy note 4 nipo Mkoa wa Kagera Bukoba je ni Tsh ngapi kwa sasa na je mna weza ni tumia mpaka hapa nilipo????
nataka s7 edge mwezi june ukifika 0688667201
Tunawakubali sn ktk ubora ila mtoe list pia ya bei nafuu ktk simu zenu
Je naweza kununua sin kwa installment? Na kama jibu ni ndio je interval ni ipi
Maoni* S4 inauzwaje
nawakubali sana mnacm nzuri
Display screen ya samsung galaxy s6 ni bei gani??
Maoni*Nataka kujua bei ya s 5 samsung galaxy
Maoni * nahitaji Samsung G N7000
Mko vizur jamani me naitaji s7 edge sh ngap
Mko vizur jamani me naitaji s7 edge sh ngap
Sijaona Samsung j5 ktk listi
Mnafanya vizur sana
Pia ni wapongeze
Kwa binafsi napenda kujua kuhusu not 5 na not edge na je sim zote mnazo tueleze vema mtwambie kama zina ingia maji au la ya ni water proof Au la?
Maoni*mbona halzijaichaji cm zenu
vipi sijaona samsung s6 na bei yake
samahani nataka kujua naweza pata A90 samsang pia naomba kujua uwezo wake zaidi
samahani jmani nawapenda sana samsung kwa huduma zenu jmani na simu yangu samsung S3 imepasuka kioo inaniuma sana inamwaka sasa ipo tu mnaweza kunisaidia kupata kikoo
Mko vizur sana named ndiyo simulator ninayoitumia isiyo na maswali mengi
Naitaj kujua gharam ya A3 Dukan
mbona mmesahau kuweka samsung galax x9plous
nilikuwa nauliza samsung j5 duos sh ngap
Cm ya s10 + sh ngap nitafuten namba 0783974462
Kwanini hamuweki security ya I cloud kama simu za apple, ili zikiibiwa zisifunguke
Nahtaji kujua bei ya samsung galaxy A10.na duka lenu hapa dar linapatkana wapi?
Soma hapa
Samsung A10 BEI TAFADHALI
Tayari swali lako limesha jibiwa
Samsung A10 BEI TAFADHALI
dukani mpya
Soma hapa
Vp kuhusu Samsung Galaxy J7 Neo!
VP bei ya Samsung A10s???
Ivi Samsung galaxy j5 duos Ni shingapi
sumsung j410F inauzwa xh ngap?
bei ya samsung j410f
Maoni*naitaji sumsung galaxy mega 2 inauzwa bei gan