LG V20 ni moja kati ya simu bora sana kutoka kampuni ya LG, simu hii ina ubora sana kwa pande zote ukianzia upande wa hardware simu hii imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu sana, pia simu hii imeongezewa programu bora ambazo zinafanya simu hii kuwa ya kisasa na yenye kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kwa ukamilifu. Ukweli ni kwamba kama wewe ni mpenzi wa android na unapenda vifaa kutoka kampuni ya LG basi hii ni simu bora na ya kisasa na yenye sifa zote bora.