Google pixel ni simu bora sana kuwa nayo kwa sasa, simu hii imevunja rekodi kwa kuwa ya kwanza kabisa kuwa na teknolojia mpya ya Google Assistance kama ile iliyoko kwenye programu ya Google Allo. Simu hii mbali na kuwa inatumia teknolojia ya hali ya juu sana simu hii inaonekana kukaa na chaji na kuwa na sifa nyingi ambazo pengine kila simu ya Android ingetakiwa kuwa nazo. Simu hii imetengenezwa na kampuni ya teknolojia ya Google na kama tunavyojua Google ndio yenye mfumo wa Android hivyo lazima simu hii itakuwa bora sana kwenye mfumo wake wa uendeshaji hivyo ni vizuri sana kuwa na simu hii