Linapokuja swala la simu bora ni wazi kuwa kila mtu ana maono yake kuhusu simu gani ni bora kwa upande wake, lakini pamoja na hayo yapo mambo kadhaa ambayo wote kwa pamoja tunaweza kujadiliana ili kuweza kujua ubora wa simu fulani kwa urahisi zaidi. Yafuatayo ni maoni yangu binafsi kuhusu simu ipi ni bora kati ya Tecno Camon X Pro na Tecno Camon 11 Pro.
Kwa kuanza labda tuanze na utangulizi mfupi, Tecno Camon X Pro na Camon 11 Pro zote ni simu simu nzuri na pia zote ni simu ambazo zinakaribiana sana kwa sifa, lakini pamoja na hayo hizi zimepishana kwenye baadhi ya mambo mbalimbali ambayo yanafanya simu hizi kutofautiana sana hasa kwa mtu anetaka kununua simu moja kati ya hizi. With that said, let’s get to it.
Muundo
Tukianza kwa nyuma Tecno Camon 11 Pro inaonekana vizuri kuliko Tecno Camon X Pro, pengine hii ni kutokana na rangi mpya ya Nebula black. Anyway simu zote mbili zimetengenezwa kwa plastiki hivyo ni vizuri sana kutumia Cover kuweza kuzuia simu isipate michubuko hasa kwenye Camon 11 Pro.
Kwa mbele kama unavyoweza kuona simu zote karibia zinafanana kwa ukubwa wa kioo lakini Camon 11 Pro imezidi kidogo kwa kuwa na kioo chenye ukubwa wa inch 6.2 tofauti na Camon X Pro ambayo inakuja na kioo cha inch 6.0. Lakini japokuwa kioo cha Camon 11 Pro ni kikubwa lakini naweza kukwambia kioo cha Camon X Pro kina sifa nzuri zaidi kuliko cha Camon 11 Pro.
Kioo cha Camon 11 Pro kina uwezo wa kuonyesha video zenye uwezo wa hadi 720p pekee huku Camon X Pro kwa upande mwingine inauwezo wa kuonyesha video za hadi 1080p hii ikiwa kwenye mfumo wa HD. Hivyo basi, kama unataka simu yenye kioo kikubwa basi unaweza kununua Camon 11 Pro na kama unataka simu yenye kioo chenye uwezo zaidi basi unaweza kununua simu ya Tecno Camon X Pro.
Sifa
Kwa upande wa sifa sidhani kama kuna haja ya kuelezea sana lakini kama ni mara yako ya kwanza hapa Tanzania Tech basi kama unavyoweza kuona Camon 11 Pro inakuja na sifa nzuri zaidi kuliko Camon X Pro. Kitu kingine ambacho ni muhimu uweze kufahamu ni kuwa Camon 11 Pro inauwezo mzuri wa kudumu na chaji kuliko Camon X Pro hii ikiwa inachangiwa na aina ya kioo cha Camon 11 Pro kwani kina mahitaji madogo ya mwanga kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa resolution.
Kwa upande mwingine Camon 11 Pro inakuja na mfumo mpya wa HiOS 4.1 wakati Camon X Pro yenyewe inakuja na HiOS 3.4, Mbali na hayo simu zote zinakuja na mfumo wa Android Oreo 8.1 na zote zinakuja na battery zenye uwezo sawa na pia simu zote zinakuja na processor zenye uwezo sawa wa Octa-core 2.0.
Camera
Kwa upande wa kamera yapo mambo mengi ya kujadiliana hapa kwani kila simu ina mapungufu yake na kila simu ina ubora wake. Tukianza kwa upande wa kamera za mbele, Simu zote zinakuja na kamera ya Megapixel 24 lakini kwenye Camon 11 Pro kamera yake ya mbele inakuja na mfumo wa AI au (Artificial Intelligence).
Kwa kuangalia kwa haraka haraka utona picha za kamera ya Selfie za Camon 11 Pro zinaonekana na mwanga zaidi wakati picha zile za Camon X Pro zinakuja na mwanga wa wastani hivyo kufanya picha za Camon X Pro kuonekana halisi zaidi. Ukiangalia picha hapo juu utaona picha moja ni mweupe zaidi na picha nyingine ni rangi ya kawaida.
Kwa upande mwingine kamera ya Selfie ya Camon 11 Pro inafanya kazi vizuri zaidi hasa pale utakapo zoom picha hizo kwani Camon 11 Pro inauwezo wa kuonyesha picha ikiwa na detals zaidi kuliko simu ya Camon X Pro. Lakini pamoja na hayo bado Camon 11 Pro inaonekana kuonyesha mwanga zaidi na kufanya picha zake za Selfie kuonekana zikiwa zime ngaa zaidi.
Kwa upande mwingine ukiwa umewasha Flash za mbele na kupiga picha za Selfie ukiwa ndani, Camon X Pro inaonekana kufanya kazi nzuri zaidi kuliko Camon 11 Pro kwa kupiga picha zenye mwanga halisi kuliko zile za Camon 11 Pro, unaweza kuangalia utofauti kwenye picha hapo chini.
Kwa upande wa kamera za nyuma Camon 11 Pro ukweli haina mpinzani kwani inajitahidi sana kupiga picha nzuri zenye mwanga sahihi ukitofautisha na Camon X Pro. Kumbuka Camon 11 Pro inakuja na kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na MP 16 na nyingine ikiwa na MP 5, Camon X Pro yenyewe inakuja na kamera moja tu ya MP 16.
Mwisho wa siku ni kweli kwamba kati ya Camon X Pro na Camon 11 Pro kwa upande wa kamera kamera ya Camon 11 Pro inaonekana kuchukua picha zenye mwanga zaidi kuliko zile za Camon X Pro. Kama wewe ni mpenzi wa Selfie basi pengine unaweza kuendelea kutumia kidogo simu yako ya Camon X Pro kwani ni kweli inauwezo wa kuonyesha picha za Selfie ambazo ni halisi zaidi.
Simu zote zinakuja na uwezo mzuri wa kuchuku video bora kwani simu zote zinakuja na uwezo wa kuchukua video za 1080p Video.
Hitimisho
Kwa kuhitimisha nadhani ni wazi kila simu hapa inakuja na kasoro yake na kila simu inakuja na mazuri yake, kilichobaki sasa ni kuangalia mfuko wako unasemaje kwani ni wazi kuwa kama una pesa zaidi ni vyema ununue simu ya Camon 11 Pro na vilevile kama huna pesa ya kutosha unaweza kununua Camon X Pro kwani nayo ni simu nzuri sana kuwa nayo.
Kwa sasa toleo la Camon X Pro linauzwa kuanzia Tsh 495,000 kupitia soko la Jumia na Camon 11 Pro yenyewe bado haijaingia maduka hapa nchini Tanzania lakini bei inakadiriwa kuanzia Tsh 500,000 na kuendelea.
Na hayo ndio mawazo yangu juu ya simu bora kati ya Tecno Camon X Pro na Tecno Camon 11 Pro, natumaini makala hii inaweza kukusaidia kufanya maamuzi sahihi unapotaka kununua simu moja kati ya hizi. Kama una maoni ushauri au kama una maswali kuhusu simu hizi basi unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.
kwahiyo techno 11 pro Tanzania lini itaingia labuda
Sasa mm nilikuwa nauliza upande wa bei wa sim ya Tecno camon11 pro pia itaingia sokoni lini
Izo sim zishafika au bado
Zipo
Vipi kuhusu Tecno camon x?
nazani zimeshafika tanzania bei zikoje mie naitaka hiyo comon x 11 pro
Maoni*JE SIMU ZOTE 2 ZINAUWEZO WA KUBADILI HANDWRITING HARD COPY KUWA SOFT COPY?