Kwa mujibu wa tovuti ya kandanda, Klabu ya soka ya Simba siku mbili zilizopita imefanikiwa kuzindua tovuti rasmi ya klabu ambayo ilianza kufanyiwa kazi tangu January ya mwaka huu na kua tayari kwa matumizi kuanzia tarehe 23 ya mwezi huu wa tano mwaka 2020.
Kulingana na muonekano unao onekana kwenye tovuti hiyo, kupitia tovuti hiyo unaweza kufanya mambo mbalimbali kama vile, kuona habari mbalimbali za klabu hiyo, ikiwa pamoja na kuona matokeo ya mechi ambazo zimechezwa hivi karibuni na habari nyingine za muhimu kuhusu klabu hiyo ya michezo ya Simba SC.
Kwa mujibu wa mtendaji wake mkuu Senzo Masingisa akiwa na msemaji wa klabu ya Simba Hajji Manara pamoja na watendaji wengine wa idara ya habari na tehama wa klabu hiyo, wamesema kwasasa ukiwa popote duniani unaweza kupata habari rasmi za klabu na historia ya klabu pamoja na vitu vyote vinavyo husiana na klabu kupitia tovuti hiyo.
Kwa mujibu wa Hajji Manara ” Tovuti hii itakua na lugha mbili yaani kiswahili na kiingereza, wale wenzangu namimi kama huelewi Kiingereza lugha ya kiswahili itakuwepo na hii inatufanya kuweka rekodi ya kua klabu ya kwanza kua na tovuti yenye lugha mbili Kiswahili na Kiingereza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.” alisema msemaji huyo wa klabu ya Simba SC.
Kama wewe ni mpenzi wa klabu ya Simba SC au unataka kuona muonekano wa tovuti hiyo mpya ya Simba basi unaweza kutembelea tovuti hiyo kupitia hapo chini.