Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Ndivyo Ilivyokuwa Siku ya Wajinga kwa Upande wa Teknolojia

Kama ulipitwa hivi ndivyo wenzetu wanavyo furahia teknolojia mpya
Ndivyo Ilivyokuwa Siku ya Wajinga kwa Upande wa Teknolojia Ndivyo Ilivyokuwa Siku ya Wajinga kwa Upande wa Teknolojia

Siku ya wajinga ni siku ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 mwezi wa nne (4), mwaka huu siku hii ilikuwa tofauti sana kwa wapenzi wa teknolojia kwani kulitoke vitu vingi mbalimbali ambavyo ukweli vimekuwa gumzo sana mpaka muda huu. Kukujuza yote yaliyotokea hapo jana hivi ndivyo siku hiyo ya wajinga ilivyokuwa kwa upande wa teknolojia.

  • 23ANDME + LEXUS

Hapa sina haja ya kuongea saanaaa hebu angalia mwenyewe eti kwa kutumia mate yako unaweza kuchagua gari la LEXUS lenye kuendana na wewe mhh.. pamoja na kulingana na harufu yako duhh.. na kuwasha gari lako au hitaji ufunguo bali unaitaji ULIMI ndio ulimi…

Advertisement

  • AMAZON PUBLISHING

Amazon nayo aikuwa nyuma siku kuu hii, siku ya jana yenyewe ilizindua AMAZON PUBLISHING. Hii ni huduma ambayo unaweza kumuita muandishi wa kitabu unaye mpenda popote pale alipo na kuja kwenye mlango wako. Yani hata kama yuko wapi muda wowote anakuja hapo hapo… mhh

  • ROKU

Kampuni ya ROKU nayo ilikuja na teknolojia mpya ya kukuwezesha kutumia TV yako kwa namna ya kipekee.. tafadhali usicheke… RUKU inakuletea Streaming Socks, Socks hizi zitakusaidia kutoshika rimoti yako kila mara na badala yake utakuwa na uwezo wa kutumia TV yako kwa kutumia soksi… uniamini..? shauri zako unapitwa na teknolojia mpya.

  • SODASTREAM

Soda stream hii ni aina mpya ya maji ya kisasa kabisa yenye uwezo wa kufanya mwili wako kuwa unajisikia vizuri na kikubwa zaidi maji haya yanakusaidia kutokuzeeka yaani mhhh yanasaidia usizeeke, kiswahili kigumu dooh.. oky maji haya nasikia tayari yanapatikana….

  • SPRINT

Sprint ni kampuni ya mtandao wa simu kama ilivyo kampuni ya Vodacom, sasa kampuni hii imeamua kuja na teknolojia mpya ya kisasa ya SPRINT BALL… Nadhani hii ni nzuri sana kwa watu wa vijijini na kama simu yako inasumbua mtandao jiandae na hii.

  • T-MOBILE

Sasa hauna haja ya kuwa na SMARTPHONE, kwani teknolojia inakimbia kiasi kwamba sasa kuna simu ya kisasa kabisa… SIMU YA KIATU. Ndio simu ya kiatu umesoma sawa.. simu hii inakupa uwezo wa kufanya mambo mengi sana ikiwa pamoja na kupiga simu pamoja na kamera yake ya mbelee ni nomaaa aisee bonge la simu mshkaji wangu hii daah we angalia mwenyewe.

Kama una maswali maoni au hata ushauri usisite kutuandikia hapo chini, kwa habari zaidi za teknolojia mpya kama hizi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku nakuahidi utopitwa na teknolojia mpya yoyote ile… NIAMINI. Any way… HERI YA SIKU YA WAJINGA…

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use