Ikiwa leo ni Julai 17, siku ya Emoji duniani au World Emoji Day kampuni ya Apple inasherekea siku hii kwa kuleta emoji mpya sabini (70) kwenye mfumo mpya wa iOS 12. Kwa mujibu wa Apple emoji zitakazo ongezwa ni pamoja na emoji za kangaroo, keki (cap cake), kasuku, kaa, embe pamoja na emoji za sura kama vile, emoji za sura kuonyesha ishara ya baridi, emoji za sura za kuonyesha kusherekea, pamoja na emoji za kuonyesha ishara ya sura ya mapenzi.
Kupitia blog yake Apple imeripoti kuwa Emoji hizi mpya zitakuwa zinapatikana kwenye mfumo mpya wa iOS 12 ambao unategemea kutoka rasmi baadae mwaka huu.
Siku ya Emoji Dunia ni likizo isiyo rasmi inayo adhimishwa Julai 17. Siku hiyo inaonekana kuwa “sherehe ya kimataifa ya emoji” na inaadhimishwa na matukio ya emoji na utoaji wa bidhaa mbalimbali za emoji. Siku hii Kuadhimishwa kila mwaka tangu mwaka wa 2014.
Kwa mujibu wa Wikipedia, siku ya emoji duniani ilibuniwa na mgunduzi wa mtandao wa Emojipedia, Jeremy Burge ambaye alibuni siku hiyo kutokana na emoji ya kalenda inayoonyesha tarehe hiyo ? kutoka kwenye simu za iPhone. Kufikia mwaka 2016, Google ilibadilisha emoji yake ya kalenda na kuweka tarehe hiyo kama ile ya kwenye iPhone huku ikiwa inaonyesha tarehe 17 Julai ambayo ndio siku ya Emoji Duniani.
Mara nyingi siku hii ya Emoji Duniani huadhimishwa kwa watu kutumiana meseji mbalimbali zenye kuonyesha emoji pekee, huku kwa makampuni pia siku hii ikitumika kuongeza aina mpya za emoji au bidhaa zinazo husiana na emoji. Mwaka 2015 kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi ilizindua PepsiMoji vifungashio na makopo ya soda yaliokuwa na emoji mbalimbali.
Unaweza kushiriki nasi siku hii ya emoji duniani kwa kutoa maoni yako kwa kutumia emoji kupitia sehemu ya maoni hapo chini ? HAPPY EMOJI DAY..