Muda mfupi uliopita Kampuni ya Samsung imezindua simu mpya ya Samsung Note 8, Bila kupoteza muda tumekuletea sifa za Samsung galaxy Note 8 ambayo imekuja ikiwa imeboreshwa zaidi.
Kwa kuanza basi ni vyema ukajua kuwa mwaka huu Samsung imeleta simu mpya ya Note 8 kwa staili ya kipekee kutokana na kuongeza ukubwa wa kioo cha simu hiyo ambacho sasa kina inch 6.3 huku kikiwa na teknolojia ya QHD+ AMOLED pamoja na Infinity display yenye 1 ratio ya 8.5:9 aspect ratio.
Kingine kikubwa Samsung imefanya maboresho ya kalamu ambayo ni maarufu kama S-Pen, kalamu hii kwa sasa imeongezewa vitu kadhaa kama vile “Screen Off Memo” sehemu ambayo itakusaidia kutumia kalamu hiyo hata kama kioo cha simu yako kimezimwa.
Kwa ufupi kabisa bila kukuchosha hizi hapandio sifa za simu mpya ya Samsung Galaxy Note 8 ambayo imetoka rasmi leo.
- Ukubwa wa Kioo – inch 6.3 3840×2160 chenye teknolojia ya Super AMOLED curved Infinity Display with 18.5:9 ratio
- Ukubwa wa Simu – 162.5mmx74.6mmx8.5mm
- Ulinzi – Iris scanner/fingerprint scanner
- Processor – Samsung Exynos 8895 CPU
- RAM – 6GB
- Kamera ya Nyuma – Zikombili zenye 12MP dual rear-facing camera,
- Kamera ya Mbele – 8MP front-facing camera
- Sehemu ya Kuchaji – USB-C connectivity,
- Sehemu ya Kuchomeka Headphone – 3.5mm headphone jack
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
- Ukubwa wa Memory ya Ndani – 64GB pia ina sehemu ya memory card (microSD expansion)
- Uwezo wa Battery – 3,300mAh battery yenye uwezo wa Fast charging, wireless charging support
- Rangi – Midnight Black, Maple Gold, Orchid Grey and Deep Sea Blue colour options.
Kwa ufupi kabisa hizo ndio sifa za simu hiyo mpya ya Note 8 kutoka kampuni ya Samsung, kwa sasa samsung imesema simu hizo zinapatikana kwa kuanza kuweka Oder na zitauzwa kwa Euro £869 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 2,300,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadili fedha vya siku ya leo, simu hii inatarajiwa kuanza kuuzwa miezi ya karibuni.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.
Natumia sumsang note8,nikitaka kufungua whatsapp inaniletea ujumbe whatsapp has stopped,mda mwingine nikipiga picha hazioneshi,ukidownload app inaishia 0%kutuma picha whatsapp inaniandikia the file you picked was not a photo,na haidownlod kitu chochote.ukiwasha na kuzima simu haioneshi samsung note8 badala yake inaonesha u-ntel
na hukubwa wa memory sio tena 64gb ni 32gb