Kampuni ya Samsung imerudi tena na toleo jipya la simu ya Galaxy J7 Prime na sasa simu hii inakuja na toleo jipya la Galaxy J7 Prime 2 (2018), Ambayo imezinduliwa huko nchini india kupitia tovuti ya Samsung nchini humo.
Simu hii inakuja na muundo wa kioo wa zamani, tofauti na ambavyo ungadhani kuwa samsung sasa inatoa simu zake zenye kioo cha Full Display kama ilivyozoeleka. Sifa nyingine za simu hii ni kama zifuatazo.
Sifa za Samsung Galaxy J7 Prime 2 (2018)
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya PLS TFT capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 1080 x 1920 pixels, 16:9 ratio (~401 ppi density)
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 (Nougat)
- Uwezo wa Processor – Octa-core 1.6 GHz Cortex-A53
- Uwezo wa GPU – Mali-T830 MP1
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 256.
- Ukubwa wa RAM – GB 3
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 13 yenye (f/1.9, 28mm) pamoja na teknolojia ya autofocus na LED flash
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye f/1.9 pamoja na teknolojia za phase detection autofocus, Geo-tagging, touch focus, face detection, panorama, HDR na LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3300 mAh battery
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.1, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gold na Rose Gold
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint kwa mbele
Simu hii ya Samsung Galaxy J7 Prime 2 (2018) inatarajiwa kuja siku za karibuni kwa bei ya dollar za marekani $247.15, sawa na shilingi za kitanzania Tsh 560,000 bila kodi. Kumbuka bei hii ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo, Bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.
bei ya samsung J7 kwa sasa ikoje?
Sumusing galax j7 ni cm yenye mvuto xana kwa muonekano wa nje hata ndani pia