Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu Sifa za Simu Mpya ya Nokia 3310 ya Mwaka 2017

Huu ndio ujio mpya wa simu mpya ya Nokia 3310
Nokia 3310 mwaka 2017 Nokia 3310 mwaka 2017

Kampuni ya nokia leo imeweza kuonyesha kurudi kwa kishindo kwa kuzindua simu zake tatu zenye kutumia Android pamoja na simu mpya ya Nokia 3310 ambayo imeboreshwa zaidi. Simu hii ambayo imezinduliwa leo imekuja na ubora pamoja na muonekano mpya wa kuvutia sana, huniamii.!! angalia video hapo chini.

Advertisement

  • Sifa za Nokia 3310

Simu hii kwa sasa imekuja na kamera ya nyuma ya Megapixel 2, ikiwa na flash ya LED vilevile simu hii inakuja na sehemu ya kuchomeka headphone ili kusikiliza redio pamoja na muziki, vilevile Nokia 3310 inakuja na memory ya ndani ya MB 32 huku ikikupa uwezo wa kuongeza ukubwa huo kwa memory card. Simu hii pia inakuja na Internet ya 2G uku ikiwa na uwezo wa kudumu na chaji kwa masaa 22 kama unaongea na simu na zaidi ya Mwezi mmoja kama hitumii kabisa.

Nokia 3310 inakuja kwa rangi nne tofauti yani njano, nyekundu, kijivu na blue simu hii imetengenezwa kwa ubora na kiukweli simu hii inavuti sana naweza kusema hii ndio simu itakayo chukua ulimwengu wa simu ndogo za Nokia kwa mwaka huu 2017. Kuhusu bei Nokia 3310 itauzwa kwa Euro €49 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 120,000 simu hii inategemewa kuingia sokoni kuanzia mwezi wa tatu hivyo kaa tayari kuipata.

Kwa habari na sifa za simu nyingine za Nokia zilizo zinduliwa leo endela kutembelea Tanzania Tech pia ili kupata kujua kuhusu simu hizo na nyingine nyingi mpya unaweza kudownload app ya Tanzania tech ili kuwa wa kwanza kupata habari zote za teknolojia.  pia usisahau kujiunga na channel yetu ya Youtube ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use