Motorola Yazindua Simu Mpya ya Moto Z2 Force Huko New York

Sifa za simu mpya ya Moto Z2 Force kutoka kampuni ya Motorola
Moto Z2 Force Moto Z2 Force

Kampuni ya Motorola kwa kushirikiana na kampuni ya lenovo huko nchini marekani walishirikiana hapo jana kuzindua simu yake mpya ya kisasa ya Moto Z2 Force, tofauti na matoleo ya mwaka uliopita simu hii kwa sasa imetoka simu moja tu na sio kama mwaka jana ambapo simu hizo zilitoka za aina tatu yaani Moto Z Force, Moto Z, pamoja na Moto Z Play.

Mwaka huu simu hii mpya ya Moto Z2 Force inakuja na muundo unaofanana na muundo wa simu za Moto Z za mwaka jana lakini muundo wa mwaka huu umeongezewa vitu kadhaa ambavyo lazima mpenzi wa simu hizi atapenda.

Advertisement

Mabadiliko hayo ni kama vile, mwaka huu simu hii imekuja na fingerprint kwenye sehemu ya chini karibia na kibonyezo cha home vilevile simu hiyo inakuja na kamera mbili kwa nyuma ambayo ndio sehemu gumzo sana kwa wapenzi wa simu hii, lakini haijaishia hapo kwa bahati mbaya simu hii inakuja bila kuwa na tundu la kuchomeka headphone maarufu kama “headphone jack” matokeo yake sasa itatumia headphone zenye mfumo wa USB.

Kwa upande wa ndani simu hii inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 835 huku ikiendeshwa na RAM ya GB 4 kwa simu za marekani na GB 6 kwa simu zinazotoka duniani kote, kwa upande wa ukubwa wa ndani simu hii pia ina utofauti kutokana na nchi kwani Moto Z2 Force za marekani zitakuja na ukubwa wa GB 64 wakati zile zinazotoka kwenda nje ya marekani zitakuwa na GB 128 hii ina maanisha simu hizo zitauzwa bei zaidi kidogo.

Simu hii ya mwaka huu inakuja na pia na battery ndogo ya 2,730 mAh ambapo simu ya mwaka huu imeonekana kuwa na battery ndogo ukilinganisha na simu za mwaka jana zilizokuwa na battery ya 3,000 mAh. Ukizingatia simu ya mwaka huu imekuja na vifaa vya pembeni maarufu kama Moto Mods ambayo lazima kwa namna moja ama nyingine vinatumia battery nyingi basi motorola kwa namna moja ama nyingine wanahitaji kubadilisha hili, kujua zaidi hizi hapa ndio sifa kamili za simu hiyo mpya ya Moto Z2 Force.

  • Kioo – 5.5-inch POLED ShatterShield 2560 x 1440 resolution 535 ppi
  • Processor – 2.35 GHz octa-core Qualcomm Snapdragon 835 Mobile Platform GPU Adreno 540
  • RAM 4 GB (U.S.) 6 GB (Rest of world)
  • Ukubwa wa Ndani – A  64 GB (U.S.) 128 GB (China) MicroSD Yes, up to 2 TB
  • Kamera za Nyuma Cameras Rear camera 1: 12 MP IMX 386 color sensor with 1.25µm pixels, f/2.0 aperture, PDAF, laser-assisted autofocus, Rear camera 2: 12 MP IMX 386 monochrome sensor with 1.25µm pixels, f/2.0 aperture, PDAF, laser-assisted autofocus
  • Kamera ya Mbele : 5 MP sensor with an f/2.2 aperture, 85-degree wide-angle lens, dual-tone flash
  • Aina ya Line – Nano-SIM Dual-SIM available in certain countries
  • Uwezo wa Mtandao – US Verizon+USC: 4G LTE CDMA (BC0, 1) GSM/GPRS/EDGE (850, 900, 1800, 1900 MHz) UMTS/HSPA+ (B1, 2, 5, 8)US Sprint:
  • Viunganishi Bluetooth 4.2, upgrade to Bluetooth 5.0 after Android O update Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac 2.4 GHz + 5 GHz with MIMO NFC Moto Mods connector
  • Aina ya USB Type-C port 3.5 mm to USB Type-C headphone port adapter
  • Sensors Mbalimbali Fingerprint, Accelerometer Ambient Light, Gyroscope, Magnetometer, Barometer, Proximity, Ultrasonic, Audio monitor
  • Uwezo wa Battery 2,730 mAh Non-removable 15W TurboPower
  • Uwezo wa Kutokuingia Maji Water resistance Water-repellent nano-coating
  • Toleo la Android 7.1.1 Nougat
  • Rangi zinazotoka Colors Super Black, Fine Gold, Lunar Grey (T-Mobile only)
  • Ukubwa, Upana na Uzito wa Simu Dimensions and weight 155.8 x 76 x 6.1 mm143 g

Na hizo ndio sifa za simu hiyo mpya ya Moto Z2 Force ambayo imetoka hapo jana ikiwa na uwezo wa tofauti pamoja na vifaa vipya vya Moto Mods ambavyo vitakusaidia kutumia simu yako kwa aina ya tofauti na kisasa.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Android Authority

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use