Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Ndio Sifa za LG V30 Simu iliyo Zinduliwa Hivi Karibuni

Zifahamu kwa undani kidogo sifa za simu mpya ya LG V30
Sifa za LG V30 Sifa za LG V30

Hivi karibuni kampuni ya LG ilitangaza kuja na simu mpya ya LG V30, Tarehe 1 mwezi huu september kampuni ya LG ilidhibitisha maneno yake kwa kuja na simu hiyo ambayo kwa namna moja ama nyingine simu hiyo ni nzuri na inao muonekano bora zaidi.

LG V30 ni moja kati ya simu ambazo ni bora kwa mwaka huu 2017, simu hii kwa muonekano inafanana na Samsung Galaxy S8 ikiwa pamoja na kioo ambacho kinafanana kabisa na simu hiyo lakini LG V30 imeongezewa vitu kibao ambavyo vinafanya simu hiyo iwe bora na nzuri zaidi hasa kwa upande wa kamera.

Advertisement

Baada ya kusema hayo moja kwa moja twende tukangalie kinachofanya simu hii kuwa bora, moja kwa moja tungalie sifa za LG V30.

  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.1.2 (inawezekana kupata toleo jipya la Android 8)
  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6 chenye teknolojia ya OLED, curved edges pamoja na kioo cha aina ya Gorilla Glass 5
  • Processor – Qualcomm Snapdragon 835
  • RAM – GB 4 (zingine zina GB 6)
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 (kwa nchi za U.S.) GB 128 (kwa nchi za Korea, na nchi zingine) pia inayo sehemu ya microSD card slot
  • Uwezo wa Battery – 3300mAh battery haitoki kwenye simu (Non-removable), ikiwa na uwezo wa Wireless charging pamoja na Quick Charge 3.0
  • Kamera za Nyuma – Ziko mbili moja yenye Mega Pixel 16 yenye teknolojia ya f/1.6, OIS, 71° FOV pamoja na nyingine yenye Mega Pixel 13 yenye teknolojia ya f/1.9, 120° FOV
  • Kamera ya Mbele – Mega Pixel 5 yenye teknolojia ya f2.2, 90° FOV
  • Uwezo wa Network – 3G, 4G au LTE
  • Uwezo wa Spika – Audio 32-bit Quad DC,
  • Uwezo wa Kinasa Sauti – High-sensitivity microphones
  • Uwezo wa Kutokuingia Maji – Water Resistance, yenye teknolojia ya IP68 water resistant pamoja na dustproof.
  • Ukubwa wa Simu – Dimensions 151.7 x 75.4 x 7.4 mm
  • Uzito wa Simu – 158 grams
  • Rangi Zinazopatikana – Cloud Silver na Moroccan Blue
  • Bei – Bado haija tangazwa rasmi lakini inakadiriwa kuwa dollar za marekani $749 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,700,000

Na hizo ndio sifa za simu mpya ya LG V30 ambayo imezinduliwa hivi karibuni kupitia mkutano mkubwa wa IFA 2017 unaoendelea huko nchini Berlin, kupata habari zaidi za mkutano huu endelea kutembelea Tanzania Tech.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : GSM Arena

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use