Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Pia Hizi Hapa Sifa za Huawei Y7 Prime (2018)

Hii hapa ndio simu ya nne iliyozinduliwa jana na Huawei.
Sifa za Simu Huawei-Y7-Prime-2018 Sifa za Simu Huawei-Y7-Prime-2018

Hapo jana kampuni ya Huawei ilizindua simu tatu mpya, simu za Huawei P20, Huawei P20 Pro pamoja na simu ya watu maalum ya Huawei Porsche Mate RS (2018), lakini kutokana na ukubwa wa bei za simu hizi kampuni ya Huawei imeangazia kwa watu wa kipato cha kawaida kwa kuja na simu mpya ya Huawei Y7 Prime (2018).

Advertisement

Simu hii haikutangazwa jana kwenye tamasha la uzinduzi, bali Huawei Y7 Prime (2018) ilizinduliwa kupitia tovuti ya Huawei. Simu hii inakuja na sifa za kawaida na pia inakuja kwa bei nafuu ukilinganisha na simu nyingine za Huawei P20 na P20 Pro.

Simu hii inakuja na sifa mbalimbali za kawaida ikiwa pamoja na Fingerprint pamoja na sehemu mpya ya AR Lens inayo fanyakazi kama sehemu ya Effect kwenye programu ya Snapchat. Sifa zingine za simu hii ya Huawei Y7 Prime (2018) ni kama zifuatazo.

Sifa za Huawei Y7 Prime (2018)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.99 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 720 x 1440 pixels, 18:9 ratio (~269 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.4 GHz Cortex-A53
  • Uwezo wa GPU – Adreno 505
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ina Megapixel 13 na nyingine inayo Megapixel 2 zikiwa na phase detection autofocus pamoja na flash ya LED flash
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Wi-Fi Direct, hotspot, Bluetooth v4.2, A2DP, LE
    pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gold na Blue
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Tatu za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
  • Ulinzi – Fingerprint (iko mbele), Face Unlock (kufungua simu kwa uso)
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G

Simu hii kwa sasa bado haijajulikana bei halisi ya simu hiyo lakini wataalamu wa mambo wanasema simu hiyo itakuwa ya bei rahisi kidogo kutokana na sifa za simu hiyo. Endelea kutembelea Tanzania Tech tuta update makala hii baada ya kupata bei halisi ya simu hii.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use