Baada ya kuzindua simu ya Huawei Y7 Prime (2018), Kampuni ya Huawei bado inaendeleza harakati za kuhakikisha watumiaji wake wanapata simu za nzuri na za bei nafuu, kuonyesha hilo hivi leo kampuni hiyo imezindua simu nyingine ya Huawei Y6 (2018). Simu hii inakuja na maboresho mengi ikiwa pamoja na kioo cha kisasa chenye teknolojia ya Full Display.
Kioo hicho cha Huawei Y6 (2018) kinakuja kikiwa na ukubwa wa Inch 5.7 pamoja na aspect ratio ya 18:9 huku kikiwa na teknolojia ya HD. Processor ya Huawei Y6 (2018) inakuja ikiwa imetengenzwa kwa processor za Snapdragon 450 ambayo ina uwezo wa octa-core CPU, yenye speed ya GHz 1.8 pamoja na GPU ya Adreno 506, sifa nyingine za Huawei Y6 (2018) ni kama zifuatazo.
Sifa za Huawei Y6 (2018)
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.7 chenye teknolojia ya S-IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 720 x 1440 pixels, 18:9 ratio (~282 ppi density)
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Quad-core 1.4 GHz Cortex-A53, Qualcomm MSM8917 Snapdragon 425 Chipest.
- Uwezo wa GPU – Adreno 308
- Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 256.
- Ukubwa wa RAM – GB 2
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5 yenye (f/1.9), LED flash
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 MP, phase detection autofocus, LED flash
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, A2DP, LE
pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB v2.0 - Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gold na Blue
- Mengineyo – Inayo Line Mbili za Dual SIM na pia inakuja na Radio FM
- Ulinzi – HAINA Fingerprint
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
Bado tarehe ya kutoka kwa Simu hii haijawekwa wazi ikiwa pamoja na bei yake lakini wataalamu wa maswala ya teknolojia wanasema tegemea kuipata simu hii kwa dollar za marekani zisizozidi $200, ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 453,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo. Kumbuka bei inaweza kuongezeka au kupungua pale bei halisi ya simu itakapo tangazwa.
Simu zenu zipo vizur sana
Iko poa
Bei cjaiona na nahitaji hiyo simu