Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Hizi Hapa Ndio Sifa za Huawei P20 na P20 Pro

Simu hizi ni bora sana kwenye upande wa kamera na kwa muonekano
Sifa za Huawei P20 Pro na Huawei P20 Sifa za Huawei P20 Pro na Huawei P20

Kampuni ya Huawei tayari imesha zindua simu zake mpya za Huawei P20 na Huawei P20 Pro, simu hizi zimezinduliwa huko nchini ufaransa na kwa mwaka huu kampuni ya Huawei imekuja na simu bora pengine kuliko simu zote zingine za toleo la Huawei P.

Advertisement

Kabla ya kuendelea, ningependa kuwa muwazi na kuweka wazi mapenzi yangu kwa simu hizi. Kwa mujibu wangu Huawei P20 Pro ni simu bora sana kuliko hata Samsung Galaxy S9, najua utakuwa una maoni yako lakini hebu twende tukangalie sifa za simu hizi pengine utakubaliana na mimi pale  mwisho wa makala hii.

Huawei P20

Tukianza na Huawei P20, hii ni simu ambayo ina mvuto sana kwa muonekano na ni simu yenye sifa nzuri lakini inatofauti kidogo na Huawei P20 Pro, Simu hii ya Huawei P20 inakuja na ukubwa mdogo zaidi ya simu ya Huawei P20 Pro, na kingine ambacho ni tofauti kwenye Huawei P20 ni kamera. Huawei P20 inayo kamera mbili kwa nyuma wakati Huawei P20 Pro inakuja na kamera nzuri tatu kwa nyuma, sifa kamili za Huawei P20 ni Kama zifuatazo.

Sifa za Huawei P20

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.8 chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 1080 x 2244 pixels, 18.5:9 ratio (~432 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.4 GHz Cortex-A73 & 4×1.8 GHz Cortex-A53)
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP12
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko kwa machaguo mawili GB 128 pamoja na GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko kwa machaguo mawili GB 6 na GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye (f/2.0, 1080p) pamoja na teknolojia ya autofocus.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye (f/1.6, 1/2.3″, 1.55 µm,, OIS) na Kamera nyingine inayo Megapixel 20 yenye (f/1.6, 27mm) pamoja na teknolojia za Leica optics, 2x lossless zoom, phase detection, laser autofocus pamoja na flash ya dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Po 3400 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Tyep C USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Blue na Twilighte
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint kwa mbele

Simu hii inatarajiwa kuingia sokoni kuanzia leo na itanza kupatikana kuanzia dollar za marekani $800 sawa na Tsh 1,809,800 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Huawei P20 Pro

Tukija upande wa Huawei P20 Pro hapa ndipo Samsung wanatakiwa kuwa makini, Simu hii inakuja na mfumo bora sana wa kamera pamoja na aina mpya ya Teknolojia ya AI ambayo inatumika kufanya picha zako kuwa nzuri na bora. Kama mwaka huu ulivyo kwenye simu nyingi, Simu hii pia imejikita zaidi kwenye kuboresha kamera, Sifa zingine za Huawei P20 Pro ni kama zifuatazo.

Sifa za Huawei P20 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.1 chenye teknolojia ya AMOLED , chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 1080 x 2244 pixels, 18.5:9 ratio (~408 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.4 GHz Cortex-A73 & 4×1.8 GHz Cortex-A53)
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP12
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye (f/2.0, 1080p) pamoja na teknolojia ya autofocus.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko tatu moja ikiwa na Megapixel 40 yenye (f/1.8, 1/1.7″, OIS, Kamera nyingine inayo Megapixel 20 yenye (f/1.6) na Kamera ya Mwisho inayo Megapixel 8 zote zikiwa na teknolojia za Leica optics, 3x optical zoom, phase detection, laser autofocus pamoja na flash ya dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Po 4000 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Tyep C USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Blue na Twilight
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Haingizi Maji wala Vumbi.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint kwa mbele

Simu hii inatarajiwa kuingia sokoni mwezi wa nne na inatarajiwa kuja kwa bei ya dollar za marekani $ 1,110 sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 2,511,597 bei hii ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo, Bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Na hizo ndio sifa za simu mpya za Huawei P20 na Huawei P20 Pro, simu hizi zimezinduliwa leo na Huawei P20 imeanza kuuzwa kuanzia siku ya leo wakati simu ya Huawei P20 Pro itapatikana baadae Aprili mwaka huu. Kwa Tanzania tutegemee kupata simu hizi mwishoni mwa mwezi wa tano au katikati. Thats it Guys hebu niambieni mnadhani Huawei P20 Pro inaweza kufananishwa na Samsung Galaxy S9 Plus..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

9 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use