Pamoja na kampuni ya HTC kufanya vibaya kwenye mauzo ya simu kwa mwaka 2017, Lakni bado kampuni hiyo imerudi tena mwaka huu na simu yake Mpya ya HTC 12 pamoja na HTC 12+.
Kuanzia mwezi wa kwanza simu hii imeonekana ikiwa gumzo sana mitandaoni huku video mbalimbali ziki ibuka na kuonyesha muonekano wa simu hiyo kabla ya kutoka kwake, lakini hadi kufikia leo kampuni ya HTC ndio imezindua simu hizo mbili na zifuatazo hizo ndio sifa za HTC 12 pamoja na HTC 12 Plus.
Sifa za HTC Desire 12
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolutiion ya 720 x 1440 pixels, 18:9 ratio (~293 ppi density)
- Mfumo wa Uendeshaji – Android Oreo 8.0
- Uwezo wa Processor – Quad-core 1.3 GHz Cortex-A53
- Uwezo wa GPU – PowerVR GE8100
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 yenye uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 400
- Ukubwa wa RAM – GB 3
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5 yenye f/2.4, 1/5″ sensor size, 1.12 µm pixel size, pamoja na uwezo wa kuchukua video za 720p
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye f/2.2, pamoja na teknolojia za phase detection autofocus, na LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 2730 mAh battery
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS
- Mengineyo – Radio FM bado haija hakikishwa kuwepo, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
- Ulinzi – Ulinzi wa kawaida Haina Fingerprint
Simu hii inategemewa kuingia sokoni siku za karibuni ikiwa na Bei ya dollar za marekani $280 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 631,932.00.
Sifa za HTC Desire 12+ (Plus)
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.0 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolutiion ya 720 x 1440 pixels, 18:9 ratio (~268 ppi density)
- Mfumo wa Uendeshaji – Android Oreo 8.0
- Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Cortex-A53
- Uwezo wa GPU – Adreno 506
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 yenye uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 400
- Ukubwa wa RAM – GB 3
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0, 1/5″ sensor size, 1.12 µm pixel size, pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ina Megapixel 13 na nyingine ina Megapixel 2 zote zikiwa na f/2.2, pamoja na teknolojia za Geo-tagging, touch focus, face detection, HDR, panorama pamoja na LED Flash
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 2965 mAh battery
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS
- Mengineyo – Radio FM bado haija hakikishwa kuwepo, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (kwa nyuma)
Simu hii ya HTC Desire 12+ Plus inategemewa kuingia sokoni siku za karibuni kwa dollar za marekani $310 sawa na Tsh 700,000. Bei zote ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo hivyo kumbuka bei inaweza kubadilika pamoja na Tanzania ukiongeza na Kodi.
Hizo ndio sifa za HTC 12 pamoja na HTC 12+ Plus simu ambayo imezinduliwa hivi leo. Nini maoni yako unaonaje simu hii, Tena ukizingatia imetengenezwa na watu wa chache kwani kampuni ya HTC mwaka jana iliwauza wafanyakazi wake kwa kampuni ya Google.