Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Honor 10

Simu hii inakuja na kamera mbili kwa nyuma zenye mfumo wa AI
Huawei Honor 10 Huawei Honor 10

Kampuni ya Huawei imerudi tena kwa mara nyingine, Wakati huu kampuni hiyo imerudi na simu ya Honor 10, Simu hii mpya inakuja na maboresho zaidi huku ikiwa kama toleo la bei rahisi la simu ya Honor 10 View ambayo yenyewe ilizinduliwa miezi michache iliyopita na kampuni ya Huawei.

Advertisement

Simu hii mpya ya Honor 10 mbali ya kuja na maboresho hayo, simu hii pia inakuja na processor ya Kirin 970 chipset, kamera mbili kwa nyuma zikiwa pamoja na mfumo wa AI au Artificial Intelligence kama zilivyo simu za Huawei P20 pamoja na Huawei P20 Pro ambazo zenyewe zilizinduliwa mwezi uliopita.

Kioo cha simu hii kinakuja kikiwa na teknolojia ya Full Display bila kusahau ukingo wa juu maalum kama notch, Kioo hicho kina ukubwa wa inch 5.84 huku kikiwa na aspect ratio ya 19:9 pamoja na teknolojia ya IPS LCD panel na resolution ya 1,080 x 2,280px (432ppi pixel density). Sifa nyingine za simu hii ni kama zifuatazo.

Sifa za Honor 10

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.84 chenye teknolojia ya IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resoluti ya 1080 x 2280 pixels (~432 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.4 GHz Cortex-A73 & 4×1.8 GHz Cortex-A53), Hisilicon Kirin 970 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP12
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko kwa machaguo mawili GB 128 pamoja na GB 64 haina sehemu ya memory card.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko kwa machaguo mawili GB 6 na GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye (f/2.0, 1080p) pamoja na teknolojia ya autofocus.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 16 (f/1.8) na Kamera nyingine inayo Megapixel 24 yenye (B/W) pamoja na teknolojia za phase detection, autofocus pamoja na flash ya dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Po 3400 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 5V/4.5A
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Tyep C USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Mirage Purple, Mirage Blue, Magic night black pamoja na Gray gull
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (kwa mbele)

Kuhusu Bei simu hii inakuja ikiwa inauzwa kwa Yuan za china CNY 2,600 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 946,000 kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania ukichanganya na kodi.

1 comments
  1. Mimi nina honor 9lite imekufa camera ya mbele na nyuma zinaweza kupatikana na kama zinaweza kupatikana gharama zake zikoje?.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use