Baada ya kuzinduliwa rasmi jana huko nchini Dubai Blackberry Motion tayari imesha toka rasmi na sasa tumesha weza kujua sifa zake kamili na tuko tayari ku-share na wewe.
Simu hii kama kawaida inakuja na mfumo wa Android na inakuja ikiwa ni simu ya ku-touch tofauti na simu ya mwaka jana ya Blackberry Key One, swali linakuja je simu hii itakuwa bora kuliko toleo hilo liliopita.?
Basi bila kupoteza muda moja kwa moja hizi hapa ndio sifa za Blackberry Motion
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.1.1 Nougat
- Ukubwa wa Kioo – inch 5.5, 1920×1080 IPS LCD 403ppi, DragonTrail Glass, Nano-diamond anti-scratch coating
- Uwezo wa Processor – Aina tatu Qualcomm Snapdragon 625 au Octa-core 2.00GHz, Adreno 506 GPU
- Ukubwa wa RAM – GB 4
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 yenye uwezo wa kutumia microSD mpaka 2TB
- Kamera ya Nyuma – 12MP (1.55 micron) f/2.0, PDAF dual-tone LED flash HDR, 4K, 30fps, 8MP f/2.2
- Kamera ya Mbele – 1.12-micron pixels, Selfie flash 1080p/30 video
- Uwezo wa Battery – 4000mAh non-removable, Charging Quick Charge 3.0
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4GLTE
- Ulinzi – DTEK security suite FIPS 140-2 Full Disk Encryption
- Uwezo wa Wi-Fi – 802.11ac, 5GHz,
- Uwezo wa Bluetooth – 4.2 LE, NFC, GPS, GLONASS
- Bei – Dollar za marekani $460 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,032,148 bei inaweza kubalika kwa Tanzania.
- Upatikanaji – Itapatikana Mwisho wa mwezi huu October kwa sasa imezinduliwa pekee Dubai.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.