Tetesi : Hizi Hapa Sifa za Awali za Samsung Galaxy Note 9

Inasemekana hizi ndio sifa na muonekano wa Galaxy Note 9
Muonekano wa Galaxy Note 9 Muonekano wa Galaxy Note 9
Muonekano wa Galaxy Note 9

Hivi karibuni kampuni ya Samsung imetangaza rasmi tarehe ya kuzindua simu yake mpya ya Samsung Galaxy Note 9. Kwa mujibu wa tweet kutoka akaunti ya Twitter ya Samsung, Galaxy Note 9 inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 9 ya mwezi wa nane mwaka huu 2018.

Update  –  Baada ya kuzinduliwa rasmi hizi hapa ndio sifa kamili za Samsung Galaxy Note 9

Advertisement

Wakati ikiwa imebaki takribani mwezi mmoja, tetesi kuhusu Galaxy Note 9 nazo zinazidi kwa wingi sana huku moja kati ya tetesi ambazo nimeona nimuhimu wewe kufahamu kwa siku ya leo ni hii ya  muonekano wa awali wa Galaxy Note 9 pamoja na sifa zake. Hata hivyo picha za muonekano huu ni moja kati ya picha ambazo zinasemekana ndio picha zenye muonekano halisi wa simu hiyo mpya ya Samsung Galaxy Note 9.

Kwa mujibu wa tetesi kutoka kwa mvujishaji anae aminika Eldar Murtazin, Galaxy Note 9 itakuja na muonekano usio pishana sana na muonekano wa Galaxy Note 8, sehemu ya nyuma ya simu hiyo ndio itakuwa na tofauti kidogo kwani sehemu ya fingerprint itakuwa imeamishwa kutoka pembeni ya kamera na kuwekwa chini ya kamera ili kuzuia kugusa na kuchafua lensi za kamera pale unapotaka kutumia sehemu ya fingerprint.

Tetesi hizo pia zinasema, Uzito wa Galaxy Note 9 utakuwa ni mkubwa zaidi kuliko ule wa Galaxy Note 8 na hiyo ni kutokana na ukubwa wa battery ya Note 9 ambayo inasemekana kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kudumu na chaji kutokana na kuwa na battery yenye 4,000 mAh ambayo inasemekana kuwezesha simu hiyo kudumu na chaji kwa siku moja nzima au siku mbili kulingana na matumizi.

Kwa upande wa ukubwa wa ndani, Galaxy Note 9 inasemekana kuja na ukubwa wa ndani wa aina tatu kati ya GB 128, GB 256 pamoja na GB 512, huku zikiwa na machaguo ya RAM kati ya GB 6 na GB 8 kama tetesi za mwezi uliopita zikivyo ainisha. Mbali na hayo kwa upande wa processor Note 9 inasemekana kutumia processor ya  Qualcomm Snapdragon 845 kwa simu za nchini China, huku simu nyingine za nje ya china zikitarajiwa kupata processor mpya za Samsung za Exynos SoC.

Wakati kukiwa hakuna tetesi za undani kuhusu Kamera za Note 9, lakini pia inasemekana zinategemewa kupata mamboresho pia huku zikoingezewa uwezo zaidi pamoja na teknolojia ya (optical image stabilization) inayo saidia kupiga picha na kuchukua video vizuri hataka kama wewe au kitu unacho chukua kiko kwenye mwendo. Mbali na hayo hakuna tetesi zaidi kuhusu uwezo wa kamera hizo.

Kwa upande wa kalamu maalum ya simu za Note kutoka kwa Samsung (S Pen), Mwaka huu inasemekana Note 9 itakuja na S pen yenye uwezo wa bluetooth pamoja na uwezo wa kufunga na kufungua simu yako kwa kutumia kalamu hiyo, Pia inasemekana Samsung itatangaza baadhi ya kazi mpya zitakazo kuwa zinafanywa na kalamu hiyo ya S Pen. Mbali na tetesi hizo, pia inasemekana kuwa kioo cha Galaxy Note 9 kitakuja na maboresho zaidi huku teknolojia ya (Always On) ikiboreshwa zaidi.

Kwa sasa hizo ndio tetesi za awali za Samsung Galaxy Note 9, Kwa habari zaidi na kujua zaidi kuhusu simu hii mpya kutoka Samsung itabidi kuendelea kusubiri hadi hapo tarehe 9 mwezi wa nane mwaka huu 2018.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use