Hivi leo kampuni ya Samsung imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Samsung Galaxy J7 Duo (2018), simu hii ambayo imezinduliwa leo huko nchini india kupitia Tovuti ya Samsung, inakuja na maboresho mapya na kamera mbili kwa nyuma kwa mara ya kwanza kwenye simu za Galaxy J7.
Mbali na maboresho ya kamera, simu hii ya Galaxy J7 Duo (2018), sasa inakuja na kioo kikubwa cha inch 5.5 ambacho kinakuja na teknolojia ya Super AMOLED na HD kikiwa na uwezo wa kuonyesha rangi za tofauti hadi rangi milioni 16.
Sifa za Samsung Galaxy J7 Duo (2018)
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 720 x 1280 pixels, 16:9 ratio (~267 ppi density)
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Octa-core 1.6 GHz Cortex-A53, Exynos 7870 Octa Chipest
- Uwezo wa GPU – Mali-T830 MP1
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 256.
- Ukubwa wa RAM – GB 4
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye (f/1.9), LED flash
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na teknolojia ya (f/1.9) na nyingine ikiwa na Megapixel 5 ikiwa na teknolojia ya (f/1.9), autofocus, LED flash
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, A2DP, LE
pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB - Rangi – Inakuja kwa rangi Mbili za Black na Gold
- Mengineyo – Inayo Line Mbili za Dual SIM na pia inakuja na Radio FM
- Ulinzi – Fingerprint (iko kwa mbele)
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
Kuhusu bei simu hii inategemewa kuingia sokoni kuanzia kesho April 12 kwa nchini india ambapo inategemewa kuuzwa kwa rupia za india INR 16,990 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 600,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo. Kama kawaida kumbuka bei inaweza kuongezeka kwa hapa Tanzania ukijumlisha na kodi.
Maoni* uwezo wa Sim hiyo itakuwa na uwezo mkubwa pia kwa watanzania wote wanao penda product za samsung watafaidika na teknolojia hiyo mpya.
msaada nilikua nauliza Tecno camon CM imethibitishwa na google maana kuna baadhi ya CM hazijathibitishwa na goolge