Mkutano wa MWC 2019 Bado unaendelea huko nchini Barcelona na sasa ni zamu ya kampuni ya LG. Kama ilivyo tegemewa kwenye mkutano huo LG nayo imezindua simu zake mpya za LG G8 ThinQ na LG G8s ThinQ, simu hizi kwa muonekano hazina tofauti sana na simu za mwaka jana 2018 za LG G7 ThinQ.
Japokuwa simu hii inafanana muonekano na simu ya mwaka jana, lakini kwenye upande wa sifa simu hii haifanani kabisa na LG G7 ThinQ. Kwanza kwa upande wa kioo LG G8 ThinQ inakuja na kioo cha inch 6.1 chenye resolution ya 3120x1440px pamoja na teknolojia ya OLED, Huku LG G8s yenyewe ikiwa inakuja na kioo kikubwa zaidi cha inch 6.2 chenye resolution ya 2248×1080 pixel, pamoja na teknolojia ya OLED.
Kwa mbele simu zote zinakuja na kamera za Selfie zenye uwezo wa Megapixel 8 huku kamera nyingine kwa pembeni yake ikiwa ni TOF kwa ajili ya kupima kiwango cha mwanga kati ya mpigaji wa picha na mpigwaji picha. Kwa nyuma simu hizi zinatofautina kwani G8 ThinQ yenyewe inakuja na kamera tatu za Megapixel 12 mbili na moja ikiwa Megapixel 16, Wakati G8s yenyewe inakuja na kamera tatu za Megapixel 12 zikiwa mbili na moja ikiwa na Megapixel 13.
Mbali na hayo kitu cha tofauti kwenye simu hizi ni teknolojia mpya ya kufungua simu hii kwa kutumia kiganja cha mkono. Kuweka uwezo wa teknolojia hii kwenye simu LG imetengeneza Sensor maalum ambayo inaweza kukusaidia kuweza kufanya mambo mbalimbali kwa kutumia kiganja choko pekee cha mkono.
Ninapo sema kiganja chako pekee hii ina maana kuwa hii itafanya kazi kama fingerprint na kiganja chako pekee ndio kitakuwa kinaweza kufanya kazi kwenye simu husika.
Mbali na hayo LG G8 ThinQ inakuja na teknolojia mpya kutoka kwenye TV za LG, ambapo kioo cha simu hiyo pia kinatumika kama Spika. Mbali ya hayo Sifa nyingine za LG G8 ThinQ na G8s ThinQ ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za LG G8 ThinQ
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.1 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1440 x 3120 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie).
- Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.8 GHz Kryo 485).
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm).
- Uwezo wa GPU – Adreno 640.
- Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – GB 6.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 8 na nyingine ni ToF.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye,f/1.5, 27mm (standard), 1.4µm, OIS, PDAF & laser AF. Nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.9, 16mm (ultrawide), 1/3.1″, 1.0µm, no AF. (Pia inasemekana baadhi ya nchi simu hii itakuja na kamera tatu).
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging na Wireless Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE, aptX HD na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO na USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector; magnetic connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Carmine Red, New Aurora Black, New Moroccan Blue.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack. Inayo teknolojia ya kuzuia maji na vumbi, IP68 dust/water proof (up to 1.5m for 30 mins).
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Bei ya LG G8 ThinQ
Kwa upande wa bei ya LG G8 ThinQ, kwa sasa bado bei yake haijatangazwa ila tegemea kupata simu hii ikiwa inauzwa kwa bei ya makadirio kati ya dollar $899 ambayo ni sawa na takribani Tsh 2,102,000 bila kodi.
Sifa za LG G8s ThinQ
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.2 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1080 x 2248 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie).
- Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.8 GHz Kryo 485)
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm).
- Uwezo wa GPU – Adreno 640.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili moja inakuja na ukubwa wa GB 64 na nyingine inakuja na ukubwa wa GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – GB 6.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 8 na nyingine ni ToF.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu moja ikiwa na Megapixel 12 yenye,f/1.5, 27mm (standard), 1.4µm, OIS, PDAF & laser AF. Nyingine ikiwa na Megapixel 13 wide na nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye 52mm (telephoto), f/2.4, 1.0µm, 2x optical zoom, OIS, PDAF.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3550 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging na Wireless Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE, aptX HD na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO na USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector; magnetic connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Carmine Red, New Aurora Black, New Moroccan Blue.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack. Inayo teknolojia ya kuzuia maji na vumbi, IP68 dust/water proof (up to 1.5m for 30 mins).
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Bei ya LG G8s ThinQ
Kwa upande wa bei ya LG G8s ThinQ, nayo bado haijatangazwa rasmi lakini tegemea kupata simu hii kwa makadirio ya dollar za marekani kuanzia $999 ambayo hii ni sawa na Tsh 2,336,000 bila kodi.
Kumbuka bei hii ni makadirio na sio bei rasmi ya simu hii. Endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi pale bei ya simu hizi itakapo Tangazwa rasmi. Kwa habari zaidi kuhusu mkutano wa MWC 2019, hakikisha unatembelea ukurasa wetu maalum ili kujua yote yanayojiri.
This is when a user comment