Kampuni ya Tecno Yazindua Camon 15 na Camon 15 Pro

Zifahamu hizi hapa sifa pamoja na bei ya Camon 15 na Camon 15 Pro
Kampuni ya Tecno Yazindua Camon 15 na Camon 15 Pro Kampuni ya Tecno Yazindua Camon 15 na Camon 15 Pro

Hatimaye kampuni ya Tecno hivi leo imetangaza ujio wa simu zake mpya za Tecno Camon 15 pamoja na Camon 15 Pro, simu hizi ni matoleo mapya ya kwanza ya simu za tecno kwa mwaka huu 2020. Simu zote mbili zimetengenezwa kwa muonekano wa kisasa huku zikiangalia zaidi kamera.

Kampuni ya Tecno Yazindua Camon 15 na Camon 15 Pro

Advertisement

Tukianza na Tecno Camon 15 Pro, simu hii inakuja na kioo kikubwa inch 6.53 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya FHD IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha picha na video za resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2340. Camon 15 Pro inakuja na kioo ambacho kimejaa simu nzima kwani simu hii haina kamera ya mbele kama zilivyo simu nyingine za Tecno zilizotangaulia.

Kampuni ya Tecno Yazindua Camon 15 na Camon 15 Pro

Simu hii inakuja na aina mpya ya kamera ya selfie ambayo ipo kwa juu ya simu hivyo kioo cha mbele ni kikubwa na haina ukingo mkubwa sana. Kamera hiyo ya selfie inakuja na uwezo wa Megapixel 32 huku ikiendeshwa na mota maalum ambapo pale mtu atakapo taka kupiga picha kamera hiyo hutokea juu ya simu hiyo na kupotea pale mtu atakapo funga programu ya kamera.

Kwa nyuma Camon 15 Pro inakuja na kamera nne zenye uwezo wa Megapixel 48, Megapixel 5, Megapixel 2 na kamera ya mwisho ikiwa pia na Megapixel 2. Kamera zote kwa pamoja zina uwezo wa kuchukua picha bora sana hasa wakati wa usiku, kutokana na teknolojia yake ya kisasa ya AI ambayo inafanya simu hizo kuongeza mwanga zaidi kwenye picha unazopiga. Sifa nyingine za Tecno Camon 15 Pro ni kama zifuatazo.

Kampuni ya Tecno Yazindua Camon 15 na Camon 15 Pro

Sifa za Tecno Camon 15

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.53 chenye teknolojia ya FHD IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.3 GHz Cortex-A53 & 4×1.8 GHz Cortex-A53).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6765 Helio P35 (12nm).
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya hadi GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 iliyopo juu ya simu inayo endeshwa na mota maalum. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Kamera za Nyuma – Zipo kamera nne, kamera moja inakuja na Megapixel 48, Megapixel 5, Megapixel 2 na kamera ya mwisho inakuja na QVGA kamera.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ice Jadeite, na Opal white
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, na proximity.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint kwa nyuma.

Bei ya Tecno Camon 15 Pro

Kwa mujibu wa tovuti ya Tecno ya nchini India, Camon 15 Pro inategemewa kuanza kupatikana kuanzia mwezi huu na simu hii inatarajiwa kuuzwa kwa rupee ya india Rs 14,999 ambayo ni takribani shilingi za kitanzania Tsh 482,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kuongeza kwa Tanzania.

Tecno Camon 15

Kwa upande Camon 15 simu hii inakuja na kioo cha inch 6.55 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD HD+ Dot-in display chenye uwezo wa resolution ya hadi pixel 720 kwa 1600. Tofauti na Camon 15 Pro, simu hii yenyewe inakuja na kamera ya mbele ambayo inakuja juu ya kioo.

Kampuni ya Tecno Yazindua Camon 15 na Camon 15 Pro

Kamera hiyo ya mbela inakuja na uwezo wa Megapixel 16 huku ikiwa na teknolojia ya AI ambayo inafanya uweze kupiga picha vizuri sana hasa wakati wa usiku. Kamera hiyo inakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 720p@30fps.

Kwa upande wa nyuma, Camon 15 inakuja na kamera nne, kamera kuu inakuja na Megapixel 48 na kamera nyingine mbili zinakuja na Megapixel 5 na Megapixel 2 huku kamera ya mwisho inawa ni QVGA . Kamera zote zinakuja na teknolojia ya Ai ambayo inawezesha kamera hizo kupiga picha vizuri sana wakati wa usiku. Sifa nyingine za Camon 15 ni kama zifuatazo.

Sifa za Tecno Camon 15

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.55 chenye teknolojia yaIPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1600 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.3 GHz Cortex-A53 & 4×1.8 GHz Cortex-A53).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6765 Helio P35 (12nm).
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya hadi GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 iliyopo juu ya kioo.
  • Uwezo wa Kamera za Nyuma – Zipo kamera nne, kamera moja inakuja na Megapixel 48, Megapixel 5, Megapixel 2 na kamera ya mwisho inakuja na QVGA kamera..
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 5000 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Shoal Gold, Fascinating Purple pamoja na Jade
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, na proximity.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint kwa nyuma.

Kampuni ya Tecno Yazindua Camon 15 na Camon 15 Pro

Bei ya Tecno Camon 15

Kwa upande wa bei kama ilivyo Camon 15 Pro, simu hii nayo pia inatarajiwa kupatikana kwanza kwa nchini India na inategemewa kuanzia rupee ya india Rs. 9,999 sawa na takribani Shilingi za kitanzania TZS 322,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Kwa sasa bado hakuna taarifa za lini simu hizi zitakuja Tanzania na bado hakuna taarifa kama simu hizi zitauzwa zote kwa pamoja kama Camon 15 na Camon 15 Pro.

https://priceintanzania.com/comparison/tecno-camon-15-vs-tecno-camon-15-pro/

1 comments
  1. Simu hizi ni nzuri.Kwa hapa Tanzania kwa mfano Mimi naihitaji naweza pata kwa muundo au utaratibu upi.natamani kuitumia nipo Mkoa ea Ruvuma wilaya ya Mbinga

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use