Katika siku kadhaa zilizopita kampuni ya Xiaomi imezindua bidhaa zake tofauti ikiwemo simu mpya ya Xiaomi Mi Note 10, simu ambayo ni bora sana kwenye upande wa kamera. Simu hii ni bora sio kwa sababu tu ya kuja na kamera ya Megapixel 108 bali pia simu hii inakuja na kamera tano.
Kwa mujibu wa DxOMark, simu hii ya Xiaomi Mi Note 10 ambayo nchini China inajulikana kama Xiaomi Mi CC9 Pro ni simu bora duniani kwa upande wa kamera. Hata hivyo simu hii inakuja na teknolojia bora kama vile HDR10 na teknolojia nyingine kama hizo. Kama unataka kujua zaidi zifuatazo ni sifa kamili za Mi Note 10.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Xiaomi Mi Note 10
Utangulizi
- Model – Mi Note 10
- Imetangazwa – 2019, November
- Itazinduliwa – 2019, December
- Upatikanaji – 2020, January
Muundo
- Vipimo – 157.8 x 74.2 x 9.7 mm (6.21 x 2.92 x 0.38 in)
- Uzito – 208 g (7.34 oz)
- Rangi – Nyeusi
Mtandao
- Uwezo wa 2G – Ndio
- Uwezo wa 3G – Ndio
- Uwezo wa 4G – Ndio
- Aina ya laini – Nano SIM
- Idadi ya laini – Laini Mbili
Kioo
- Aina ya kioo – Super AMOLED
- Ukubwa – inch 6.47
- Uwiano – 1080 x 2340 pixels
- Idadi ya pixel – 398 ppi density
- Ulinzi – Corning Gorilla Glass
Media
- FM Radio – Inayo Radio
- Earphone Jack – Inayo sehemu ya headphone
Kamera
- Idadi ya Kamera – Kamera Moja ya Tano
- Kamera kuu – 108 MP, f/1.7, (wide), 1/1.33″, 0.8µm, PDAF, Laser AF, OIS
- Kamera ya pili – 5 MP, f/2.0, (telephoto), 1.0µm, PDAF, Laser AF, OIS, 5x optical zoom
- Kamera ya tatu – 12 MP, f/2.0, 50mm (telephoto), 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, Laser AF, 2x optical zoom
- Kamera ya nne – 20 MP, f/2.2, 13mm (ultrawide), 1/2.8″, 1.0µm, Laser AF
- Kamera ya tano – 2 MP, f/2.4, 1/5″, 1.75µm (dedicated macro camera)
- Video – 2160p@30fps, 1080p@30fps
- Flash – LED flash
- Idadi ya selfie – Kamera moja
- Selfie kamera – 32 MP, f/2.0, 0.8µm
- Video – 1080p@30fps
Mfumo Endeshaji
- OS – Android 9.0 (Pie)
- Mfumo wa simu – Android One
Sifa za Ndani
- Chipset – Qualcomm SDM730 Snapdragon 730G (8 nm)
- CPU – Octa-core (2×2.2 GHz Kryo 470 Gold & 6×1.8 GHz Kryo 470 Silver)
- GPU – Adreno 618
- RAM – 8 GB
- Hifadhi – 128/256 GB
- Memory kadi – Bado haijathibishwa
- Sensors – Fingerprint (under display, optical), accelerometer, gyro, proximity, compass
Viunganishi
- Bluetooth – 5.0, A2DP, LE, aptX HD
- Wi-fi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac, dual-band, Wi-Fi Direct
- Wi-fi Hotspot – Ndio
- USB – 2.0, Type-C 1.0 reversible connector
- GPS – A-GPS, GLONASS, GALILEO, BDS
- NFC – Ndio
Battery
- Aina ya Battery – Li-Ion (Lithium Ion)
- Uwezo – 5260 mAh battery
- Muundo – Non-removable
- Fast Charging – Yes, 30W
Bei ya Xiaomi Mi Note 10
Kwa upande wa bei simu hii inategemewa kuanza kupatikana kuanzia tarehe 15 mwezi huu, huku ikiwa inauzwa kwa Euro €549 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania TZS 1,396,000 bila kodi. Hata hivyo inasemekana kuwa simu hii inakuja na toleo la Mi Note 10 Pro ambalo litauzwa kwa Euro €649 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania TZS 1,651,000 bila kodi, toleo hilo litakuwa na sifa zilizo fanana isipokuwa RAM itakuwa ni GB 8 na uhifadhi wa ndani utakuwa ni GB 256.
Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania, kwa sababu ya kupanda au kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha ikiwa pamoja na kodi. Kama unataka kujua pale simu hii itakapofika hapa Tanzania hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku ikiwa pamoja na kipengele cha simu janja.