Kampuni ya Xiaomi hivi karibuni imekuja na ingizo jipya kwenye soko la smartphone ingizo hilo ni simu mpya ya Xiaomi Mi Mix 3 simu ambayo imekuwa ikizungumziwa sana siku za karibuni.
Moja kati ya sababu kubwa za simu hii kuzungumziwa sana ni pamoja na sababu za simu hii kuja na mfumo wa kamera kama ule wa Oppo Find X, mfumo ambao kamera inakuwa kwenya kifuniko ambacho kinaweza (kuslide) kwa kupanda juu unapo piga picha na kushuka chini pale unapofunga programu ya kamera. Pia sababu nyingine ya simu hii kuwa gumzo ni ukubwa wa RAM wa simu hii ambayo hadi sasa hii ndio simu ya pili kwa kuwa na RAM ya GB 10 baada ya simu ya Xiaomi Black Shark Helo ambayo nayo imezinduliwa siku za karibuni.
Kwa upande wa simu hii ya Xiaomi Mi Mix 3 yenyewe inakuja na kioo cha inch 6.4, kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED na kwa mujibu wa Xiaomi simu hii inakuja na kioo ambacho ni Full Display kwa asilimia 93, mbali na hayo simu hii inakuja na kamera mbili kwa mbele kamera ambazo utaweza kuziona pindi tu utakapo slide kwa kwenda juu kifuniko maalum kilicho tengenezwa kwa sumaku. Kamera hizo za mbele zinakuja na uwezo wa Megapixel 24 MP pamoja na Megapixel 2.
Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili pia ambazo kamera zote zinakuja na uwezo wa Megapixel 12 kwa kila kamera. Tofauti na hayo, simu hii ya Xiaomi mi Mix 3 inakuja na processor ya Snapdragon 845 ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 6, GB 8 au GB 10 pamoja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 128 na GB 256. Simu hii inakuja bila sehemu ya kuweka memory card hivyo ukubwa huo wa ndani ndio utakaopata wakati wa kutumia simu hii. Sifa nyingine za Xiaomi Mi Mix 3 ni kama zifuatazo.
Sifa za Xiaomi Mi Mix 3
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.39 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~403 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie).
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver).
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset.
- Uwezo wa GPU – Adreno 630.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za tatu simu moja inakuja na GB 128, nyingine GB 256 pamoja na nyingine inakuja na GB 512 zote zikiwa hazina uwezo wa Memory Card.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina tatu moja ikiwa na RAM ya GB 6, GB 8 na nyingine ikiwa na GB 10.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili moja inakuja na Megapixel 24 yenye 1/2.8″, 0.9µm na nyingine inakuja na megapixel 2 ambayo hii ni depth sensor.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenyef/1.8, 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, 4-axis OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye 1/3.4″, 1.0µm, huku zote zikiwa zinasadiwa na HDR, panorama na LED Flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3200 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging (Quick Charge 4.0+).
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi moja nne za Jade Green, Sapphire Blue, Onyx Black, Forbidden City Blue (kwa toleo lenye RAM ya GB 10)
- Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Bei ya Xiaomi Mi Mix 3
Kwa upande wa bei Xiaomi Mi Mix 3 simu hii inakuja kwa matoleo tofauti ambayo yanakuja kwa bei tofauti, Mi Mix 3 yenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani GB 128 inauzwa kwa Yuan ya China CNY 3,299 sawa na Tsh 1,090,000 bila kodi. Xiaomi Mi Mix 3 yenye RAM ya GB 8 na ukubwa wa GB 128 inauzwa Yuan ya China CNY3,599 ambayo ni sawa na Tsh 1,189,000 bila kodi. Simu yenye ukubwa wa ndani wa GB 256 na RAM ya GB 8 inauzwa kwa Yuan CNY3,999 sawa na Tsh 1,321,000 bila kodi.
Kwa upande wa Xiaomi Mi Mix 3 yenye RAM ya GB 10 na ukubwa wa ndani wa GB 256 yenyewe itauzwa kwa Yuan ya China CNY4,999 sawa na Tsh 1,652,000 bila kodi. Simu hizi zinategemewa kuanza kupatikana kuanzia mwezi ujao Novemba.