Habari njema kwa wapenzi wa game, kampuni ya Xiaomi hivi karibuni imetangaza kuzindua simu yake mpya ya Xiaomi Black Shark Helo. Simu hii ni matokeo ya toleo la kwanza la simu ya Xiaomi Black Shark ambayo iliyozinduliwa miezi sita iliyopita.
Kwa sasa simu hii mpya ya Xiaomi Black Shark Helo inakuja na maboresho kadhaa kama vile kioo kikubwa cha inch 6.01 chenye resolution ya 1080 x 2160 pixel. Mbali na hayo Black Shark Helo inakuja na processor ya Snapdragon 845 ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 6, GB 8 pamoja na toleo lingine ambalo linakuja na RAM ya GB 10. Simu hii inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 256 ambayo bado haijajulikana kama inauwezo wa kuongezewa kwa memory card.
Kwa upande wa kamera Xiaomi Black Shark Helo inakuja na kamera mbili kwa nyuma huku kamera moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine ikiwa na Megapixel 20. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya selfie yenye uwezo wa Megapixel 20.
Kwa upande wa Game Xiaomi Black Shark Helo inakuja na vitufe maalum ambavyo kwa matoleo yenye simu hii yenye RAM ya GB 6 na GB 8 utapata kitufe cha upande mmoja na kwa simu yenye RAM ya GB 10 utapa vitufe viwili vya kushoto na kulia kwaajili ya kucheza game, ili kukupa uwezo zaidi wa kucheza game simu hii inakuja na battery kubwa ya 4000 mAh yenye teknolojia ya Quick Charge 3.0.
Mbali na hayo simu hii inakuja na programu maalum ya Gamer Studio inakusaidia kuweza kufanya simu hiyo kucheza game kwa urahisi zaidi. Kingine Xiaomi Black Shark Helo inakuja na spika nzuri zenye kutoa sauti nzuri pake unapocheza game.
Mbali ya yote hayo simu hii inaendeshwa na mfumo wa Android 8.0 Oreo, Sifa nyingine za simu hii mpya ya Xiaomi Black Shark Helo ni kama zifuatazo.
Sifa za Xiaomi Black Shark Helo
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.01 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, na uwiano wa 18:9 ratio (~402 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo).
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 385 Silver).
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset.
- Uwezo wa GPU – Adreno 630.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za mbili simu moja inakuja na GB 256 na nyingine inakuja na GB 128 zote zikiwa zikiwa hazina uwezo wa Memory Card.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina tatu moja ikiwa na RAM ya GB 6, GB 8 na nyingine ikiwa na GB 10.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20 yenye f/2.2, 1.0µm.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 1.25µm, dual pixel PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 20 yenye f/1.8, 1.0µm, AF, 2x optical zoom zote zikiwa zinasadiwa na Dual-LED dual-tone flash, HDR, panorama
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh battery battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W (Quick Charge 3.0).
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Black.
- Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Bei ya Xiaomi Black Shark Helo
Kwa upande wa bei simu hii ya Xiaomi Black Shark Helo inatarajiwa kuuzwa kwa Yuan CNY3,199 sawa na Tsh 1,056,000 simu yenye RAM ya GB 6 na kwa upande wa simu yenye RAM ya GB 8 yenyewe itauzwa ka Yuan ya china CNY3,499 ambayo ni sawa na Tsh 1,155,000. Kwa upande wa simu yenye RAM ya GB 10 yenyewe bado haijatagazwa bei yake.
Kiongoz mpaka sasa enda campuni ya Tecno ikafa kisa mfumo wa simu kama hii tujipange kwel kumiliki mijombo kama hii je tanzania imefika hiyo Simu kwel au ipo nchi gani kwa sasa
Tanzania zitapatikana