Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya LG Yazindua Simu Mpya za W10, W30 na W30 Pro

Fahamu sifa na bei ya simu mpya za LG W10, LG W30 pamoja na LG W30 Pro
Kampuni ya LG Yazindua Simu Mpya za W10, W30 na W30 Pro Kampuni ya LG Yazindua Simu Mpya za W10, W30 na W30 Pro

Kampuni ya LG hivi leo imetangaza ujio wa series mpya za simu za LG W Series, simu ambazo zinakuja zikiwa na zimelenga zaidi soko la watumiaji wa simu za bei nafuu.

Advertisement

Kupitia tamasha lake la uzinduzi lililo fanyika leo huko nchini India, LG imezindua simu zake za kwanza za series hiyo za LG W10, LG W30 pamoja na LG W30 Pro. Simu hizi zote zinakuja zikiwa zinauzwa kwa bei nafuu sana tofauti na Series nyingine za simu za LG.

Kwa upande wa sifa, Simu hizi mpya za LG W Series zote zinakuja na mfumo wa Android 9.0 Pie, pia zinakuja na battery zenye uwezo unaofanana wa 4000mAh battery, uwezo ambao unasemekana kufanya simu hizo kudumu na chaji kwa muda wa siku moja nzima kulingana na matumizi yako.

Kampuni ya LG Yazindua Simu Mpya za W10, W30 na W30 Pro

Vile vile simu za LG W10 na LG W30 zinakuja na processor zinazo fanana za Mediatek MT6762 Helio P22 processor ambayo inakuja na uwezo wa Octa-core 2.0 GHz, huku ikisaidiwa na RAM ya GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 32 kwenye simu zote za LG W10 na W30. Mbali na hayo simu hizi zote zinakuja na fingerprint kwa nyuma pamoja na ulinzi wa kutambua uso au Face unlock. Sifa nyingine za simu hizi ni kama zifuatavyo.

Sifa za LG W10

Kampuni ya LG Yazindua Simu Mpya za W10, W30 na W30 Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.19 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6762 Helio P22 (12 nm).
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezwa na memory card ya microSD ya hadi GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye flash ya LED
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13, PDAF na kamera nyingine ikiwa na Megapixel 5, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, 4.2, A2DP, HD, LE
    na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Tulip Purple na Smokey Grey.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya LG W10

Kwa upande wa bei LG W10 inategemewa kuingia sokoni kwanza kwa nchini india kwa rupee ya india INR 8,999 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za kitanzania 299,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kutokana na kodi.

Sifa za LG W30

Kampuni ya LG Yazindua Simu Mpya za W10, W30 na W30 Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.26 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6762 Helio P22 (12 nm).
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezwa na memory card ya microSD ya hadi GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12, PDAF na kamera nyingine ikiwa na Megapixel 13 na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, 4.2, A2DP, HD, LE
    na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Thunder Blue, Platinum Grey, Aurora Green.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya LG W30

Kwa upande wa bei LG W30 inategemewa kuingia sokoni kwanza kwa nchini india kwa rupee ya india INR 9,999 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za kitanzania 333,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kutokana na kodi.

Sifa za LG W30 Pro

Kampuni ya LG Yazindua Simu Mpya za W10, W30 na W30 Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.21 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×1.8 GHz Kryo 250 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 250 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM632 Snapdragon 632 (14 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 506.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezwa na memory card ya microSD ya hadi GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12, PDAF na kamera nyingine ikiwa na Megapixel 8 na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 5, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, 4.2, A2DP, HD, LE
    na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Pine Green, Denim Blue na Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya LG W30 Pro

Kwa upande wa bei, LG W30 Pro inategemewa kuingia sokoni baadae mwezi huu na kwa sasa bado bei ya simu iyo haija tangazwa rasmi. Kama unataka kujua zaidi kuhusu simu hii akikisha unaendelea kutembelea ukurasa huu tutaweka bei ya simu hii pindi itakapo tangazwa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use