Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Spark 3 na Spark 3 Pro

Hizi hapa sifa kamili pamoja na bei ya simu mpya za Tecno Spark 3
Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Spark 3 na Spark 3 Pro Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Spark 3 na Spark 3 Pro

Kampuni ya Tecno tayari imesha zindua simu zake mpya za Tecno Spark 3 na Tecno Spark 3 Pro, tofauti na simu za mwaka jana za Tecno SPARK 2, mwaka huu simu hizi zinakuja kwa aina mbili tofauti huku tofauti yake kubwa ikiwa ni ukubwa wa ROM. Kama ilivyokuwa kwenye tetesi, kampuni ya tecno imezindua simu hizi huko nchini Kenya na tayari sifa zake kamili na bei zinapatikana.

Kwa upande wa Tecno Spark 3, yenyewe inakuja na kioo cha inch 6.2 chenye teknolojia ya HD+ simu hii pia ni ya kwanza kabida kuja na mfumo wa Android 9.0 Pie, mfumo unao saidiwa na processor ya Quad-core MediaTek MT6761 na RAM ya GB 2. Sifa nyingine za Tecno spark 3 ni kama zifuatazo.

Advertisement

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Spark 3 na Spark 3 Pro

Sifa za Tecno Spark 3

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core CPU (4×1.3, GHz Cortex-A53).
  • Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek MT6761
  • Uwezo wa GPU – Mali G71.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 2
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.9, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye f/2.2. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3500 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ocean Blue na Charcoal Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G na 3G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Tecno Spark 3

Kwa upande wa bei ya Tecno Spark 3, inapatikana kupitia maduka mbalimbali ya Tecno hapa Tanzania pamoja na kupitia makampuni ya simu kwa Tsh 280,000 pamoja na kodi.

Kwa mujibu wa Techweez, Kwa upande wa Simu mpya ya Tecno Spark 3 Pro, yenyewe nayo pia imezinduliwa nchini Kenya na pia kama nilivyo kwambia awali, simu hizi hazina tofauti kwenye sura bali tofauti kubwa iko kwenye sifa za ndani. Tecno Spark 3 Pro inakuja na uwezo wa 4G wakati Tecno Spark 3 inakuja na uwezo wa mtandao wa 3G. Pia Spark 3 Inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 16 wakati Spark 3 Pro inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 32 Sifa nyingine za Tecno Spark 3 Pro ni kama zifuatazo.

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Spark 3 na Spark 3 Pro

Sifa za Tecno Spark 3 Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core CPU, 2.0 GHz
  • Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek MT6761
  • Uwezo wa GPU – Mali -.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 2
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.9, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye f/2.2. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3500 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ocean Blue na Charcoal Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Tecno Spark 3 Pro

Kwa upande wa bei ya Tecno Spark 3 Pro, simu hii pia imesha ingia sokoni hapa Tanzania na inapatikana kupitia maduka mbalimbali ya Tecno pamoja na maduka ya makampuni ya simu (Tigo)  kwa Shilingi za kitanzania Tsh 333,000 pamoja na kodi.

Na hizo ndio sifa pamoja na bei ya Tecno Spark 3 na Tecno Spark 3 Pro, simu hizi kwa Tanzania bado hazijaja hivyo kama unataka kujua kuhusu mapunguzo ya bei ya simu hizi zitakapo kuja hapa nchini Tanzania.

May 09 2019 : Makala imeongezwa kuonyosha bei ya Tecno Spark 3 na Spark 3 Pro baada ya kuzinduliwa rasmi hapa nchini Tanzania.

6 comments
  1. Nimejaribu kutumia application ya jiotv lakini kila nikijisajili haifunguki naomba msaada wenu ahsanteni sana.

  2. Nna simu ya techno spark 3 hua inazima yenyewe ghafla na baadae nikiiwasha inaendelea na kaz kama kawaida he shida ni nini ?na nifanye nini ili kutatua hili tatizo?

  3. Maoni*naitwa Joseph nipo Zanzibar mie naomba mtutumie vioo vya simu Aina ya spark3 model kb7j navijatufikia

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use