Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya TECNO Pouvoir 3

Zifahamu kwa undani hizi hapa ndio sifa na bei ya TECNO Pouvoir 3
Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya TECNO Pouvoir 3 Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya TECNO Pouvoir 3

Kampuni ya TECNO hapo siku ya jana imezindua simu yake mpya ya Pouvoir 3 huko nchini Nigeria, Simu hii mpya ni toleo la maboresho la simu ya Pouvoir 2 ambayo ilitoka rasmi mwaka jana 2018.

Kama unavyojua simu za Tecno Pouvoir zime tengenezwa maalum kwa ajili ya wale wanaopenda simu zenye uwezo wa kudumu na chaji hivyo Pouvoir 3 inakuja na battery kubwa ya 5000 mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa zaidi ya siku moja kulingana na matumizi yako.

Advertisement

Mbali na hayo Pouvoir 3 inakuja na Kioo cha inch 6.2 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, kioo ambacho kina kuja na resolution ya 720 x 1500 pixels. Kwa mbele Pouvoir 3 inakuja na kamera ya Megapixel 13 ambayo inasaidiwa na Flash ya LED kuweza kupiga picha za selfie vizuri hasa wakati wa usiku.

Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya TECNO Pouvoir 3

Kwa nyuma simu hii pia inakuja na kamera ya Megapixel 13 ambayo nayo inasaidiwa na Flash mbili za LED, Vile vile Pouvoir 3 inaendeshwa na processor ya Mediatek MT6739 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 2 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 16 au GB 32. Sifa nyingine za Tecno Pouvoir 3 ni kama zifuatazo.

Sifa za TECNO Pouvoir 3

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixels
    (~294 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.2GHz,
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6739 (32 nm).
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8100
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili simu moja yenye GB 16 na nyingine inakuja na GB 32 Simu zote zinakuja zikiwa na uwezo wa kuongezewa na Memory Card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 2
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 13, yenye LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye Dual LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 5000mAh
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za City Blue, Midnight Black, Champagne Gold
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya TECNO Pouvoir 3

Kwa upande wa bei Tecno Pouvoir 3 inakuja ikiwa inauzwa kwa takribani shilingi za kitanzania Tsh 350,000. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika pale simu hii itakapo zinduliwa hapa nchini Tanzania.

3 comments
  1. Naomba kuuliza mm natumia simu aina ya Tecno povour 3 air lakini nikiwa nataka kupiga simu huwa inazima mwanga hata km bado sijaisogeza sikioni, kitu ambacho nashindwa hata kuweka round spika, hata kukata pindi nimalizapo kuongea, je ninatakiwa nifanyej?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use