Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya TECNO Phantom 9

Hizi hapa sifa kamili pamoja na bei ya simu mpya ya TECNO phantom 9
Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya TECNO Phantom 9 Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya TECNO Phantom 9

Kama wewe ni mpenzi wa simu za TECNO basi habari njema kwako kwani kampuni ya TECNO hivi karibuni imezindua rasmi simu mpya ya TECNO Phantom 9 huko nchini Nigeria. Simu hii ni toleo jipya la simu za Phantom, Simu ambazo ndio simu zenye sifa bora zaidi kwenye matoleo yote ya simu za TECNO.

Kama ilivyokuwa kwenye tetesi, simu hii inakuja na sifa zinazofanana kabisa na zile zilizotangazwa kwenye makala iliyopita. Kwa ufupi, TECNO Phantom 9 inakuja na kioo kikubwa cha Inch 6.4 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED kioo ambacho pia kina uwezo wa resolution ya hadi pixel 1080 x 2340.

Advertisement

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya TECNO Phantom 9

Kioo hicho kwa mbele kinakuja na ukingo wa juu ambao una julikana kama water drop notch, ukingo ambao unatumika kuhifadhi kamera ya mbele ya Selfie ya Megapixel 32, kamera hiyo inasaidiwa na Flash mbili zilizopo kwa mbele karibia na kona za simu hiyo. Vilevile kwenye kioo hicho kunakuja teknolojia mpya ya Fingerprint ambayo inaruhusu mtumiaji kufunga simu yake kwa kutumia alama za vidole.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya TECNO Phantom 9

Kwa nyuma, TECNO Phantom 9 inakuja na kamera tatu ambazo zina Megapixel 16, Megapixel 8 pamoja na Megapixel 2, kamera zote zinasaidiwa na teknolojia ya AI pamoja na HDR pamoja na teknolojia nyingi ambazo zitafanya picha zako kuonekana vizuri sana.

Kwa upande wa sifa za ndani Phantom 9 inakuja ikiwa inaendeshwa na processor ya Mediatek MT6765 Helio P35 (12 nm), yenye uwezo wa CPU ya Octa-core 4×2.35 GHz Cortex-A73 & 4×2.0 GHz Cortex-A53). Procesor hii inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 128, ukubwa huu unaweza kuongezwa na memory card ya MicroSD Card yenye uwezo wa hadi GB 500.

Pia TECNO Phantom 9 itakuja na mfumo mpya wa Android 9.0 (Pie), mfumo ambao juu yake kuna mfumo wa Tecno HiOS v5.0, Sifa nyingine za TECNO Phantom 9 ni kama zifuatazo.

Sifa za TECNO Phantom 9

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya TECNO Phantom 9

[aps_product_specs id=”33938″]

Bei ya TECNO Phantom 9

Kwa mujibu wa TECNO, Kwa upande wa bei simu hii mpya inatarajiwa kuingia sokoni hapa Tanzania siku za karibuni, Na inategemewa kupatikana kwa bei ya makadirio kuanzia shilingi za kitanzania Tsh 750,000 hadi Tsh 720,000 Kumbuka bei inaweza kubadilika kutokana na mahali unapo nunua simu hii.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use