Kampuni ya Sony imerudi tena na toleo jipya la simu ya Sony Xperia XA2 Plus, Sony Xperia XA2 Plus ni toleo jipya la simu za Sony Xperia XA2 na Sony Xperia XA2 Ultra ambazo zilizinduliwa mapema mwaka huu kwenye mkutano wa CES 2018.
Kwenye toleo hili jipya kampuni ya Sony imefanya baadhi ya maboresho huku mabadiliko makubwa yakiwa kwenye kioo cha simu hiyo. Kwa upande mwingine Xperia XA2 Plus bado inakuja na processor ya Snapdragon 630 kama matoleo yaliyotangulia.
Tukirudi kwenye kioo chenyewe, Xperia XA2 Plus ni simu ya kwanza kwenye mfululizo wa matoleo ya simu za Sony XA2 kuja na kioo chenye uwiano wa 18:9. Kioo hicho cha LCD kinakuja kikiwa na ukubwa wa Inch 6 huku kikiwa na teknolojia ya Full HD, mbali na hayo kioo hicho kimetengenezwa kwa ubora na kuwekewa ulinzi wa Gorilla Glass 5. Sifa nyingine za Xperia XA2 Plus ni kama zifuatazo.
Sifa za Sony Xperia XA2 Plus
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.0 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, 18:9 ratio (~402 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Octa-core 2.2 GHz Cortex-A53, Qualcomm SDM630 Snapdragon 630 chipset.
- Uwezo wa GPU – Adreno 508
- Ukubwa wa Ndani – Ziko mbili moja ikiwa na GB 64 na nyingine ikiwa na GB 32 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
- Ukubwa wa RAM – Ziko mbili moja ina RAM ya GB 4 na nyingine ina RAM ya GB 6
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye (f/2.4, 1/4″).
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 23 yenye f/2.0, 24mm, 1/2.3″), PDAF na LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3580 mAh battery yenye teknolojia ya – Fast battery charging (Quick Charge 3.0).
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Silver, Black, Gold na Green.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Ulinzi wa Fingerprint (Kwa nyuma)
Bei ya Sony Xperia XA2 Plus
Hii hii imezinduliwa rasmi hapo siku ya jana na kampuni ya Sony, lakini bado hakuna taarifa kamili kuhusu bei yake, kama unataka kujua bei ya simu hii endelea kutembelea makala hii tutaweka bei pindi simu hii itakapo toka rasmi.