Wakati tukiwa kwanza ndio tuko siku ya pili ya mkutano wa MWC 2019, kampuni mbalimbali bado zinaendelea kuzindua simu zake mpya na kwa sasa ni zamu ya kampuni ya Sony.
Kampuni hiyo kupitia mkutano huo imetangaza ujio wa simu zake mpya za Sony Xperia 1, Xperia 10 na Xperia 10 Plus, huku simu za Xperia 10 zikisemekana kuwa za daraja la kati (premium mid-range) wakati Xperia 1 ikisemekana kuwa ndio simu ambayo ni flagship kutoka Sony kwa mwaka huu 2019.
Anyway, As usually bila kupoteza muda twende moja kwa moja tukaangalie sifa, muonekano na bei za simu hizi mpya kutoka kampuni ya Sony.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Sony Xperia 10
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.0 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1080 x 2520 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie).
- Uwezo wa Processor – Octa-core 2.2 GHz Cortex-A53.
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM630 Snapdragon 630 (14 nm).
- Uwezo wa GPU – Adreno 508.
- Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili za moja inakuja na RAM ya GB 3 au GB 2.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 8.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 13 yenye, PDAF. Nyingine ikiwa na Megapixel 5.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 2870 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging na Wireless Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS, GLONASS na USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector; USB Host.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Carmine Red, New Aurora Black, New Moroccan Blue.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Pembeni).
Bei ya Sony Xperia 10
Kwa upande wa bei Xperia 10 bado haija tangazwa rasmi ila tegemea kupata simu hii kuanzia dollar za marekani $499 sawa na Tsh 1,168,000 bila kodi. Kumbuka bei hii ni ya makadirio hivyo inaweza kubadilika pale bei halisi itakapo tangazwa.
Sifa za Sony Xperia 10 Plus
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.5 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1080 x 2520 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie).
- Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Kryo 260.
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 (14 nm).
- Uwezo wa GPU – Adreno 509.
- Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili za moja inakuja na RAM ya GB 4 au GB 6.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0, 24mm (wide), 1/4″, 1.12µm.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye, f/1.8, 27mm (wide), 1/2.8″, 1.25µm, PDAF. Nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.4, 53mm (telephoto), 1/4″, 1.12µm, PDAF, 2x optical zoom.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging na Wireless Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS, GLONASS na USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector; USB Host.
- Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Navy, Silver, Gold.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Pembeni).
Bei ya Sony Xperia 10 Plus
Kwa upande wa bei Xperia 10 Plus nayo bado haijatangazwa rasmi bei yake ila unaweza kuipata simu hii kwa bei ya makadirio kuanzia dollar za marekani $399 ambayo hii ni sawa na Tsh 937,000 bila kodi. Kumbuka bei hizi ni makadirio hivyo bei hizi zinaweza kubadilika pale bei halisi itakapo Tangazwa rasmi.
Sifa za Sony Xperia 1
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.5 chenye teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1644 x 3840 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie).
- Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.8 GHz Kryo 485).
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm).
- Uwezo wa GPU – Adreno 640.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 128 na nyingine GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – GB 6.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0, 1/4″, HDR na uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps (5-axis gyro-EIS).
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera atu moja ikiwa na Megapixel 12 yenye, f/1.6, 26mm (wide), 1/2.6, predictive Dual Pixel PDAF, 5-axis OIS. Nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye f/2.4, 52mm (telephoto), 1/3.4″, predictive Dual Pixel PDAF, 5-axis OIS. Nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye f/2.4, 16mm (ultrawide), 1/3.4″.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3300 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging na Wireless Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS, GLONASS na USB 3.1, Type-C 1.0 reversible connector; USB Host.
- Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Gray, Purple, White.
- Mengineyo – Haina Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint (rear-mounted), accelerometer, gyro, proximity, barometer, compass, color spectrum.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
Bei ya Sony Xperia 1
Kwa upande wa bei, Xperia 1 nayo bei yake bado haijajulikana ila tegemea kupata simu hii kuanzia dollar za marekani $999 ambayo hii ni sawa na Tsh 2,343,000 bila kodi. Kumbuka bei hii ni makadirio hivyo inaweza kubadilika pale bei halisi itakapo tangazwa rasmi.
Na hizo ndio simu mpya za Sony Xperia ambazo zimezinduliwa siku ya leo kwenye mkutano wa MWC 2019, Bado kampuni ya Sony inaendelea kutambulisha bidhaa mbalimbali endelea kuwa nasi tutakupa taarifa zaidi kuhusu bidhaa mpya kutoka kampuni hiyo, Kwa taarifa zaidi kuhusu simu hizi za sasa unaweza kusoma zaidi hapa.
https://www.tanzaniatech.one/mwc-2019/
This is a comment