Baada ya kuangalia sifa pamoja na bei ya Samsung Galaxy S20 na Galaxy S20 Plus, sasa moja kwa moja twende tuangalie sifa za simu nyingine ya Samsung Galaxy S20 Ultra 5G. Tofauti na matoleo yaliyopita, Galaxy S20 Ultra inakuja na sifa bora zaidi huku ikiwa ndio toleo bora zaidi kwenye simu zote hizi za mpya za Galaxy S20.
Tukianza na kioo, Galaxy S20 Ultra 5G inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.9 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Dynamic AMOLED, kama zilivyo simu nyingine za S20 simu hii pia inakuja na uwezo mara mbili zaidi wa kufanya kazi kwa haraka pale mtu anapo gusa yani kioo hicho yani 2X capacitive touchscreen. Mbali na hayo kioo hicho kinakuja na uwezo wa resolution ya hadi pixel 1440 kwa 3200 pamoja na uwiano au aspect ratio ya 20:9.
Kwa juu ya kioo hicho kuna tundu la kamera ya mbele ambayo inayokuja na uwezo wa Megapixel 40, huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K. Kamera hiyo pia ina uwezo wa Auto-HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za Dual video call. Mbali na kamera hiyo, kwenye kioo hicho cha Galaxy S20 Ultra kunayo sehemu ya ulinzi ya fingerprint ambayo inapatikana chini ya kioo.
Kwa upande wa nyuma Galaxy S20 Ultra inakuja na muundo mpya kabisa huku ikiwa ni kamera ambazo sasa zimewekwa kwenye mtindo mpya, Galaxy S20 Ultra 5G inakuja na kamera nne kwa nyuma huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 108 ambayo ni wide lens, na kamera nyingine tatu zikiwa ni Megapixel 48 ambayo ni telephoto lens na kamera nyingine ikiwa na Megapixel 12 ambayo yenyewe ni ultrawide lens.
Kamera ya mwisho inakuja na Megapixel 0.3 ambayo ni TOF 3D (depth lens), huku kwa pamoja kamera zote zikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 8K sawa na kusema Galaxy S20 Ultra 5G ina uwezo wa kuchukua video za hadi 3240p@30fps.
Sifa za Samsung Galaxy S20 Ultra 5G
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.9 chenye teknolojia ya Dynamic AMOLED 2X capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 3200 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0
- Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.73 GHz Mongoose M5 & 2×2.60 GHz Cortex-A76 & 4×2.0 GHz Cortex-A55) – Global.
- Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 990 (7 nm+) – Global.
- Uwezo wa GPU – Mali-G77 MP11 – Global.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu, yenye GB 128, GB 256 na GB 512, ukubwa huu unaweza kuongezewa kwa memory card.
- Ukubwa wa RAM – GB 12
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 40 yenye f/2.2, 26mm (wide), 1/3.2″, 1.22µm, Dual Pixel PDAF na uwezo wa video hadi 2160p@30/60fps, 1080p@30fps.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 108, yenye f/1.8, 26mm (wide), Dual Pixel PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 48, yenye f/2.0, (telephoto), PDAF, OIS, 3x hybrid optical zoom, nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye f/2.2, 13mm (ultrawide), AF, Super Steady video pamoja na Megapixel 0.3 ambayo ni TOF 3D, (depth). Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 5000 mAh.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.2, Type-C 1.0 reversible connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi za Cosmic Grey, Cloud Blue, na Cloud Pink.
- Mengineyo – Inayo Radio FM (kwa baadhi ya simu za USA na Canada), Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi yaani IP68 dust/water resistant (up to 1.5m for 30 mins).
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G na 5G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint Chini ya Kioo (under display, ultrasonic).
Bei ya Samsung Galaxy S20 Ultra 5G
Kwa mujibu wa Samsung, Samsung Galaxy S20 Ultra 5G inategemewa kuingia sokoni kuanzia mwezi wa tatu mwaka huu 2020 na bei ya simu hii inategemewa kuanzia dollar za marekani $1,399 kwa toleo lenye GB 128, hii ikiwa na sawa na takribani shilingi za kitanzania TZS 2,233,000 bila kodi. Kwa toleo lenye GB 512, tegemea kupata simu hii kwa dollar za marekani $1,599 ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania TZS 3,233,000 bila kodi.
Kumbuka bei hizi zinaweza kuongezeka kwa Tanzania kutokana na kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha ikiwa pamoja na kodi.