Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Samsung India Yazindua Samsung Galaxy On8

Samsung yazindua Galaxy J8 kama toleo la Galaxy On8
Samsung-Galaxy-On8 Samsung-Galaxy-On8

Kampuni ya Samsung kupitia tovuti ya Flipkart imetangaza kuzindua simu yake mpya ya Samsung Galaxy On8, Simu hii ni toleo la bei rahisi la simu ya Samsung Galaxy J8 (2018) kwani sifa pamoja na muundo unafanana kabisa na simu ya Galaxy J8 iliyozinduliwa miezi miwili iliyopita. Tofauti iliyopo kati ya simu hii ya Galaxy On8 na Galaxy J8 ni bei.

Sifa za Samsung Galaxy On8

Advertisement

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6 chenye teknolojia ya Super AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1480 pixels, 18.5:9 ratio (~274 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Cortex-A53, Qualcomm SDM450 Snapdragon 450 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 506
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye f/1.9, LED flash
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 16 yenye uwezo wa (f/1.7,) na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye (f/1.9), autofocus, pamoja na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black na Blue
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Micro-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), Face Detection (Kufungua kwa Kutambua Uso).

Bei ya Samsung Galaxy On8

Simu hii ya Galaxy On8 itakuja ikiwa inauzwa kwa Rupee ya India Rs. 16,990 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 567,000 bila kodi. Kumbuka kwa hapa Tanzania bei ya simu hii inaweza kubadilika kutokana na kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

1 comments
  1. kwa india wanajitaidi kutoa simu nzuri tena za bie rahisi
    niliona kama kuna tecno 1 hivi ni itel ya india na tecno
    kwanzia camon hadi toleo la f6 na kuendelea.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use