Hatimaye baada ya Tetesi za muda mrefu, leo kampuni ya Samsung mda mchache uliopita imezindua simu mpya ya Samsung Galaxy Note 9, simu hii inakuja na mabadiliko kadhaa pamoja na muonekano kama ilivyokuwa kwenye tetesi mbalimbali. Mbali na hayo Note 9 inakuja na battery kubwa ya 4,000mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji siku moja nzima kulingana na matumizi.
Kingine cha muhimu kujua kuhusu simu hii mpya ni SPen, hii ni kalamu maalum ya Simu za Note ambayo sasa inakuja na maboresho mengi kama tulivyosema kwenye tetesi za hapo awali. SPen inakuja na mfumo mpya wa Bluetooth ambao unaweza kutumia kuendesha simu yako ya Galaxy Note 9, mambo ambayo unaweza kufanya ni pamoja na kupiga picha pamoja na kucheza video za youtube moja kwa moja kwa kutumia kalamu hiyo bila kugusa simu hiyo.
Kalamu hiyo pia inaweza kufanya mambo mengi zaidi ya kwa kalamu hiyo ambayo samsung imesema siku sio nyingi itawaruhusu wabunifu wa programu kutengeneza programu mbalimbali ambazo pia zitakuwa zinaweza kuendeshwa kwa kutumia kalamu hiyo. Vilevile kalamu hiyo inachaji kwa kutumia simu yako na utairudisha kwenye sehemu yake kwenye simu ya Galaxy Note 9 na itajichaji kwa haraka ndani ya sikunde 40 au pungufu. Sifa nyingine za Galaxy Note 9 ni kama zifuatazo.
Sifa za Samsung Galaxy Note 9
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 2960 pixels, na uwiano wa 18.5:9 ratio (~514 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.7 GHz Mongoose M3 & 4×1.8 GHz Cortex-A55) – EMEA au Octa-core (4×2.7 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver).
- Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9810 Octa – EMEA au Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset.
- Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP18 – EMEA au Adreno 630.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 128, nyingine GB 512 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja ina RAM ya GB 8 na nyingine ina RAM ya GB 6.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/1.7, 25mm, 1/3.6″, 1.22µm, AF yenye uwezo wa kuchukua video za 1440p@30fps.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.5-2.4, 26mm, 1/2.55″, 1.4µm, dual pixel PDAF, OIS na kamera nyingine pia inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 52mm, 1/3.6″, 1µm, AF, OIS, 2x optical zoom.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging (Quick Charge 2.0).
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO. USB ya Type-C 3.1 reversible connector, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Metallic copper, Lavender purple, Ocean blue na Midnight black.
- Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP68 dust/water proof (maji ya urefu wa 1.5m kwa dakika 30), pia Inakuja na Samsung DeX kwaajili ya kutumia simu yako kwenye kompyuta.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Iris scanner, fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer, heart rate, SpO2
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), na Ulinzi wa kutambua uso na macho (Iris Scanner).
Bei ya Samsung Galaxy Note 9
Kwa upande wa bei simu hii itakuja kwa bei tofauti kulingana na ukubwa wa ndani wa simu yenyewe, Galaxy Note 9 ya GB 128 itauzwa kwa dollar za marekani $1,000 sawa na Tsh 2,282,000 bila kodi, Vilevile Galaxy Note 9 ya GB 512 yenyewe itauzwa kwa dollar za marekani $1,250 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 2,852,000 bila kodi. Kumbuka bei zote hizi ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo, hivyo kwa Tanzania bei inaweza kubadilika kulingana na viwango vya kubadilisha fedha vya siku husika pamoja na kodi.
Simu zote hizi zitapatikana rasmi kuanzia tarehe 24 mwezi huu wa nane huku kwa sasa ukiwa na uwezo wa kutoa oda kupitia tovuti za Samsung.