Galaxy A9 (2018) Simu ya Kwanza Yenye Kamera 4 Kwa Nyuma

Baada ya simu yenye kamera 3, Sasa Samsung imekuja na simu yenye kamera 4
Galaxy A9 (2018) Simu ya Kwanza Yenye Kamera 4 Kwa Nyuma Galaxy A9 (2018) Simu ya Kwanza Yenye Kamera 4 Kwa Nyuma

Hayawi sasa yamekuwa, Kampuni ya Samsung hivi leo imefanya tamasha la uzinduzi wa simu yake mpya ya kwanza ya Samsung Galaxy A9 (2018) yenye uwezo wa kamera nne kwa nyuma. Simu hii ambayo ilikuwa kwenye tetesi siku chache zilizopita hivi leo imezinduliwa rasmi huko Kuala Lumpur nchini Malaysia. Simu hii inafanana kidogo kwa sifa na Galaxy A7 ambayo yenyewe inakuja na kamera (3) tatu kwa nyuma.

Simu hii inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.3 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED ambacho pia kinakuja na resolution ya 1080 x 2220 pixel. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Megapixel 24 yenye f/2.0, Kamera nyingine zilizobaki ambazo ziko kwa nyuma zinakuja na Megapixel 8, Megapixel 10, Megapixel 24 pamoja na Megapixel 5.

Advertisement

Kamera ya kwanza yenye Megapixel 8 yenyewe inatumika zaidi kuchukua picha kwa upana, kamera ya pili yenye Megapixel 10 hii ni Telephoto na kamera yenye Megapixel 24 hii ndio kamera ya kawaida na kamera ya mwisho ya Megapixel 5 hii ni depth ambayo inachukua picha vizuri hasa wakati wa usiku.

Mbali na kamera simu hii inakuja na matoleo mawili ambayo matoleo yote yanakuja na ukubwa wa ndani wa GB 128 ambayo matoleo hayo yanatofautiana kwenye upande wa RAM kwani kuna toleo lenye RAM ya GB 6 na kuna toleo lenye RAM ya GB 8. Simu hii inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 660 yenye uwezo wa octa-core (4x 2.2GHz + 4x 1.8GHz) pamoja na mfumo wa Android 8.0 (Oreo) ambao juu yake unakuja na mfumo wa Samsung Experience 9. Sifa nyingine za Samsung Galaxy A9 (2018) ni kama zifuatavyo.

Sifa za Samsung Galaxy A9 (2018)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.3 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2220 pixels, na uwiano wa 18.5:9 ratio (~392 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Kryo 260 & 4×1.8 GHz Kryo 260)
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 (14 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 512.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 64 na nyingine inayo GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na GB 8
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 24 yenye f/1.7, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.4, 13mm, nyingine inakuja na Megapixel 10 yenye f/2.4, (telephoto), 2x optical zoom huku kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3800mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Caviar Black, Lemonade Blue na Bubblegum Pink.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Samsung Galaxy A9 (2018)

Simu hii mpya ya Galaxy A9 (2018) inatagemewa kupatikana kuanzia mwezi ujao kweye nchi mbalimbali, kuhusu bei bado haijawekwa wazi na kampuni ya Samsung, Kama unataka kujua zaidi hakikisha unaendelea kutembelea ukurasa huu pia tovuti ya Tanzania Tech kwa ujumla.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use