Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A8 Star

Fahamu bei ya simu mpya ya Samsung Galaxy A8 Star
Sifa na bei ya galaxy a8 star Sifa na bei ya galaxy a8 star

Kampuni ya Samsung bado inaendelea kuzindua simu mpya kila siku, hivi karibuni umesikia Samsung ikizindua simu mpya ya Note 9, lakini kama haitoshi hivi karibuni kupitia soko la mtandaoni la Amazon Samsung imetangaza ujio wa simu mpya ya Samsung Galaxy A8 Star.

Simu hii ina utofauti kidogo na simu za Galaxy A8 na Galaxy A8 Plus, Galaxy A8 Star inakuja na kioo cha inch 6.3 chenye teknolojia ya Super AMOLED Infinity display, ambacho pia kina resolution ya 1080 x 2220 pixels. Simu hii pia inakuja na processor ya Snapdragon 660 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64.

Advertisement

Kwa upande wa kamera Galaxy A8 Star inakuja na kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Magepixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 24, huku kwa mbele ikiwa na kamera kwaajili ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 24. Sifa nyingine za Samsung Galaxy A8 Star ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy A8 Star

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.3 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2220 pixels, na uwiano wa 18.5:9 ratio (~392 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Kryo 260 & 4×1.8 GHz Kryo 260).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 512.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya hadi GB 512.
  • Ukubwa wa RAM –  RAM ya GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye f/2.0, 20mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 24 yenye f/1.7 na nyingine inakuja na Megapixel 16 yenye f/1.7 PDAF. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3700 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE, EDR pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO. USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili Black na White.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Samsung Galaxy A8 Star

Kwa upande wa bei Samsung Galaxy A8 Star inapatikana kwa nchini india kwa Rupee INR 34,990 ambayo ni sawa na Tsh 1,141,000 bila kodi. Simu hii pia inapatikana kwa nchini china kwa jina la Galaxy A9 Star ambayo bei yake ni Yuan CNY 2,999 ambayo ni sawa na Tsh 1,003,000 bila kodi.

Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha vya siku husika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use