Galaxy A7 (2018) Simu ya Kwanza ya Samsung Yenye Kamera 3

Simu hii inakuja na sifa nzuri na inauzwa kwa bei nafuu zaidi
Sifa na bei ya Samsung Galaxy A7 (2018) Sifa na bei ya Samsung Galaxy A7 (2018)

Samsung imekuwa ni moja kati ya kampuni za simu zenye kutoa simu nyingi sana kwa mwaka mzima, Hivi karibuni Samsung imezindua simu mpya za Galaxy J4 Plus na J6 Plus ambazo bado zinatarajiwa kuingia sokoni siku za karibuni.

Wakati ikiwa bado tunasubiria simu hizo kuingia sokoni, Samsung imerudi tena na simu mpya ya Galaxy A7 (2018) ambayo hii ni ya kwanza kabisa kuja na uwezo wa kamera tatu kwa nyuma. Mpaka sasa kulikuwa hakuna simu yoyote ya Samsung yenye kamera za idadi hiyo lakini Galaxy A7 (2018) sasa ndio imeweza kushikilia taji hilo.

Advertisement

Samsung Galaxy A7 (2018) inakuja na kioo chenye ukubwa wa inch 6 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED display chenye uwezo wa resolution ya 1080 x 2220 pixel. Simu hii pia inakuja na uwezo wa processor yenye uwezo wa octa-core 2.2GHz CPU ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 au GB 6, Galaxy A7 (2018) inakuja na ukubwa wa ndani tofauti kati ya GB 64 na GB 128.

Simu hii mpya ya Samsung inakuja na kamera tatu kwa nyuma huku kamera moja ikiwa na Megapixel 24, nyingine ikiwa na Megapixel 8 na nyingine ya mwisho ikiwa na Megapixel 5 zote zikiwa zinasaidiwa na Flash ya LED Flash. Sifa nyingine za Samsung Galaxy A7 (2018) ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy A7 (2018)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2220 pixels, na uwiano wa 18.5:9 ratio (~411 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.2 GHz Cortex-A53
  • Aina ya Processor (Chipset) – Bado Haijajulikana.
  • Uwezo wa GPU – Bado Haijajulikana.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 64 na nyingine inayo GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 24 yenye f/1.7, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.4, 13mm na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3300 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, blue, gold na pink.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inayo uwezo wa kuzuia maji na vumbi IP68 (maji ya mita 1.5 kwa dakika 30).
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Pembeni).

Bei ya Samsung Galaxy A7 (2018)

Kwa mujibu wa Samsung, upande wa bei Samsung Galaxy A7 (2018) inatarajiwa kupatikana kwa barani ulaya na Asia kuanzia October 11 ambapo bei ya simu hii inasemekana itakuwa ni Euro €350  ambayo ni sawa na Tsh 941,000 bila kodi. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika kutokana na ciwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use