Baada ya kampuni ya Samsung kuzindua simu mpya za Galaxy A30 na Galaxy A50 mwezi uliopita, Hivi leo kampuni hiyo imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Samsung Galaxy A20.
Simu hii mpya ya Galaxy A20 inakuja na kioo cha inch 6.4 chenye resolution ya 720 x 1560 pixels, pamoja na teknolojia ya Super AMOLED. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera moja ya Megapixel 8 yenye uwezo wa kurekodi video za 1080p@30. Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili, kamera moja inakuja na Megapixel 13 na nyingine inakuja na kamera ya Megapixel 5.
Mbali na kamera simu hii inaendeshwa na processor ya Exynos 7884 Octa, ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 32, ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa kutumia Memory Card hadi ya GB 512. Sifa nyingine za Galaxy A20 ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Samsung Galaxy A20
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (2×1.6 GHz & 6×1.35 GHz).
- Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 7884 Octa (14 nm).
- Uwezo wa GPU – Mali-G71.
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – GB 3.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.9, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ocean Blue na Charcoal Black.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
Bei ya Samsung Galaxy A20
Kwa upande wa bei, kwa mujibu wa tovuti ya Samsung ya nchini urusi Galaxy A20 inategemewa kuanza kupatikana nchini humo kwa Ruble RUB 13,990 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 520,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kuongezeka kwa Tanzania kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.
Nikitaka kujua kama Samsung Galaxy a20 yangu ni original
Nimeipenda
Nikihitaji kujua ni originally nafanyaje
Nimeipenda je kwa hapa dar naipataje?
Maoni*nimeipenda! mwanza naipataje?