Kampuni ya Xiaomi ambayo iko mbioni kuja barani Afrika, hivi karibuni imezindua simu yake mpya ya bei rahisi ya Redmi Go, Simu hii inakuja ikiwa na historia ya kuwa simu ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya Xiaomi kutumia mfumo wa Android Go.
Kwa mujibu wa The Verge, simu hii ya Xiaomi inakuja ikiwa inatumia mfumo wa Android 8.0 (Oreo Go edition) hivyo ni wazi kuwa simu hii itakuwa na RAM isiyozidi GB 1, kwa upande mwingine Redmi Go inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 425 yenye uwezo wa Quad-core 1.4 GHz ambayo inasaidiawa na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 8.
Kwa sababu ni simu ya bei rahisi Redmi Go inakuja na kamera za kawaida za Megapixel 5 kwa mbele na kwa nyuma inakuja na Kamera ya Megapixel 8, simu hii inakuja na kioo cha inch 5.7 ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD pamoja na resolution ya 720 x 1280 pixels, sifa nyingine za Redmi Go ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Redmi Go
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya HD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 540 x 960 pixels, na uwiano wa 116:9 ratio (~220 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo Go)
- Uwezo wa Processor – Quad-core 1.4 GHz Cortex-A53.
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm MSM8917 Snapdragon 425 (28 nm).
- Uwezo wa GPU – Adreno 308.
- Ukubwa wa Ndani – GB 8 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya hadi GB 128.
- Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 1
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 yenye HDR, panorama na LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery Inayotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Wi-Fi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. micro USB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black na Blue
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM, Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Accelerometer na proximity.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Haina Fingerprint.
Bei ya Redmi Go
Kama nilivyo kwambia hapo awali Redmi Go ni simu ya bei nafuu na kwa sasa simu hii inauzwa dollar za marekani $90 ambayo hii ni sawa na takribani shilingi za Tanzania 210,000 bila kodi. Kwa sasa simu hii bado haija tangazwa kama inakuja Afrika ila inategemea kupatikana siku za karibuni huko barani Ulaya.