Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Razer Yazindua Razer Phone 2 Simu Mpya Kwaajili ya Game

Simu nyingine kutoka Razer maalum kwaajili ya Game
Sifa na bei ya Razer Phone 2 Sifa na bei ya Razer Phone 2

Kama wewe ni mpenzi wa game basi lazima jina Razer sio jina geni kwenye macho yako, hii ni kampuni ambayo inajihusisha na utengenezaji wa vifaa kwaajili ya Game kama vile kompyuta, laptop, headphone pamoja na simu za mkononi (Smartphone).

Mwaka jana (2017) kampuni ya Razer ilizindua simu ya kwanza ya Razer Phone na hapo siku ya jana kampuni hiyo imerudi tena na toleo la pili la simu hiyo. Razer Phone 2 inakuja na mabadiliko kadhaa ukilinganisha na toleo la mwaka jana, simu hii ya Razer Phone 2 inakuja na kioo cha inch 5.7 kilichotengenezwa kwa IGZO LCD panel chenye uwiano wa 16:9, kioo cha simu hii pia kina mwanga zaidi kuliko kile cha toleo la kwanza kwani kwa mujibu wa Razer kioo cha Razer Phone 2 kina mwanga zaidi kwa asilimia 50 zaidi hadi kufikia nits 580.

Advertisement

Mbali na kioo simu hii ya Razer Phone 2 inakuja processor ya Snapdragon 845 chipset ambayo inakuja na mfumo wa kupooza processor hiyo maarufu kama vapor chamber cooling system mfumo ambao unasaidia kuppoza simu hii pale unapokuwa unacheza game kwa muda mrefu. Processor ya simu hii inasaidiwa na RAM ya GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64, kama GB 64 haitoshi unaweza kuongeza ukubwa wa simu hii kwa kutumia sehemu ya Memory Card.

Kwa upande battery simu hii inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa 4000mAh yenye teknolojia ya Quick Charge 4.0+ pamoja na fast Qi wireless charging ambayo inafanya simu hii kujaa chaji kwa haraka. Sifa nyingine za Razer Phone 2 ni kama zifuatavyo.

Sifa za Razer Phone 2

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.72 chenye teknolojia ya IGZO IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 2560 pixels, na uwiano wa 16:9 ratio (~513 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) inatagemewa kupata Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 (10 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 630.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – RAM GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 ikiwa na f/2.0.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 25mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, dual pixel PDAF, OIS na kamera nyingine ikiwa pia na Megapixel 12 yenye f/2.6, 1/3.1″, 1.0µm, 2x optical zoom Huku ikiwa inasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 24W (Quick Charge 4+) na Wireless fast charging 15W.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Black.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja ya Nano-SIM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi IP67 (inakaa kwa dakika 30 kwenye maji yenye urefu wa mita 1).
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa pembeni).

Bei ya Razer Phone 2

Razer phone 2 inapatikana kuanzia siku ya leo kwa kutoa oda maalum kwa dollar za marekani $800 sawa na Tsh 1,831,000 bila kodi, Pia unaweza kupata toleo maalum la Razer Phone 2 lenye Satini kwa dollar za marekani $900 sawa na Tsh 2,060,000. Vilevile pia unaweza kupata vifaa mbalimbali vya simu hii kama chaji isiyokuwa na waya (Wireless Charger) kwa dollar $100 sawa na Tsh 229,000 bila kodi. Pia unaweza kupata kava kwa dollar $50 sawa na Tsh 116,000 bila kodi pamoja na screen protector kwa dollar $20 sawa na Tsh 46,000 bila kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use