Hivi karibuni kampuni ya Xiaomi ilitangaza kuwa brand yake ya Poco au Pocophone itakuwa ikijitegemea kama brand moja na itakuwa ikitoa simu zake zenyewe tofauti na hapo awali. Siku chache baada ya kutangazwa hayo kampuni ya Poco leo imetoa simu yake ya kwanza chini ya brand hiyo, Poco X2 ni simu mpya ya kabisa kutoka kampuni ya Poco na ya pili baada ya Poco F1.
Simu hiyo mpya ya Poco X2 imezinduliwa huko nchini India na inategemea kupatikana kwanza kwenye soko la Flipkart la nchini India. Simu hii inakuja ikiwa na kioo cha inch 6.67 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD ambacho pia kina kuja na resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2400. Kioo hicho kinalindwa na teknolojia ya ulinzi wa kioo ya Corning Gorilla Glass 5.
Kwa upande wa sifa za ndani, Poco X2 inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 730G (8 nm) ambayo inakuja na CPU yenye uwezo wa hadi Octa-core (2×2.2 GHz Kryo 470 Gold & 6×1.8 GHz Kryo 470 Silver). CPU hiyo inasaidiwa na RAM ya hadi GB 8 huku ikiwa na toleo lingine lenye RAM ya GB 6. Poco X2 inakuja na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 256 huku ikiwa na toleo lingine lenye uhifadhi wa GB 128. Sifa nyingine za Poco X2 ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Poco X2
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.67 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2400.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0
- Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz Kryo 470 Gold & 6×1.8 GHz Kryo 470 Silver).
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM730 Snapdragon 730G (8 nm).
- Uwezo wa GPU – Adreno 618.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu tatu moja ikiwa na GB 64, nyingine GB 128 na nyingine ikiwa na GB 256 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya microSDXC.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili za GB 8 na GB 6
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili, kamera moja ikiwa na Megapixel 20 yenye f/2.2, 27mm (wide), 1/3.4″, 0.8µm na kamera nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye f/2.4, 1/5″, 1.75µm, depth sensor.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 64, yenye f/1.9, 26mm (wide), 1/1.7″, 0.8µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8, yenye f/2.2, 13mm (ultrawide), 1/4.0″, 1.12µm, nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye f/2.4, 1/5.0″, 1.75µm (dedicated macro camera) na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2 yenye f/2.4, 1/5.0″, 1.75µm, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual-LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4500 mAh.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi za Atlantis Blue, Matrix Purple, na Phoenix Red.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Accelerometer, proximity.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint kwa pembeni.
Bei ya Poco X2
Kwa upande wa bei, kwa mujibu wa Flipkart Poco X2 inatarajiwa kuuzwa kwa rupee ya india INR15,999 sawa na shilingi TZS 519,000 kwa toleo lenye ukubwa wa ndani wa GB 64 na RAM ya GB 6. Toleo lenye uhifadhi wa GB 128 na RAM ya GB 6 liatauzwa kwa rupee ya india INR16,999 sawa na Shilingi za Tanzania TZS 552,000 bila kodi. Toleo la mwisho la Poco X2 lenye RAM ya GB 8 na uhifadhi wa GB 256 litauzwa kwa rupee ya India INR19,999 sawa na Shilingi za Kitanzania TZS 648,000 bila kodi.
kwa hapa Tanzania eisha fika? nimeopenda