Hivi karibuni kampuni ya Oppo ilizindua simu yake mpya ya Oppo R17, lakini baada ya kuzindua simu hiyo, kampuni ya Oppo imerudi tena na toleo la maboresho la simu hiyo linaloitwa Oppo R17 Pro. Simu hii inakuja na maboresho mengi sana ukilinganisha na toleo la kwanza la R17.
Simu hiyo mpya ya Oppo R17 inakuja na processor ya Snapdragon 710 chipset ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 128. Kioo cha simu hii kina ukingo wa juu maarufu kama top notch, kioo hicho kina ukubwa wa Inch 6.4 kilicho tengenezwa kwa Super AMOLED ambacho pia kina resolution ya 1080 x 2340 pixels.
Mbali na hayo, Oppo R17 Pro inakuja na kamera ya mbele yenye uwezo wa Megapixel 24, huku kwa nyuma simu hii ikiwa inakuja na kamera tatu moja ikiwa na Megapixel 20, nyingine ikiwa na Megapixel 12 na nyingine ikiwa ni TOF 3D stereo camera, ambazo hizi mara nyingi zinakuwaga mbele ya simu kwaajili ya kufanya kazi ya Face Unlock. Kwa mujibu wa Oppo kamera hiyo itakuwa inatumika kwaajili ya kupiga picha za 3D.
Tofauti na Oppo Find X ambayo haina Fingerprint, simu hii ya Oppo R17 Pro inakuja na sehemu hiyo ya Fingerprint chini ya Kioo maarufu kama under-display fingerprint sensor. Sifa nyingine za Oppo R17 Pro ni kama zifuatazo.
Sifa za Oppo R17 Pro
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~402 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver).
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM710 Snapdragon 710 Chipset.
- Uwezo wa GPU – Adreno 616.
- Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa haina uwezo wa kuongezewa na memory card.
- Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 8
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 25 yenye f/2.0, 20mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.5-2.4, 26mm, 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, OIS na nyingine inakuja na Megapixel 20 yenye f/2.6, AF na nyingine ni TOF 3D stereo camera, ambayo inatumika kupiga picha za 3D. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya Dual-LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3700 mAh battery, yenye teknolojia ya Fast battery charging: yenye uwezo wa kujaza battey hiyo hadi asilimia 40% ndani ya dakika 10 (SuperVOOC Flash Charge 5V/10A 50W)
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE, EDR pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB 3.1, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Stream Blue.
- Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Mbele Kwenye Kioo).
Bei ya Oppo R17 Pro
Kwa upande wa bei, Oppo R17 Pro inakuja ikiwa inauzwa kwa Yuan ya China CNY 4,299 ambayo ni sawa na Tsh 1,427,000 bila kodi. Simu hii itaanza kupatikana kuanzia katikati ya Mwezi kumi kwa nchini China pekee. Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi kuhusu simu hiyo kuja kwenye nchini nyingine, endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha pindi simu hii itakapo fika nchini Tanzania.
mimi nataka kujua has a kati ya oppo R9m na ifinix zero 4 plus ipi borax aid ya nyingine kabla sijafanya maamuzi
iko poa sana
alwayz oppo wako vizur kuliko infinix