Kampuni ya Oppo Yazindua Simu Mpya ya Oppo R17

Zifahamu hizi hapa sifa na bei ya simu mpya ya Oppo R17
Kampuni ya Oppo Yazindua Simu Mpya ya Oppo R17 Kampuni ya Oppo Yazindua Simu Mpya ya Oppo R17

Baada ya kampuni ya oppo kuzindua simu mpya ya Oppo Find X, Hatimaye hivi karibuni kampuni ya Oppo imerudi tena na simu mpya ya Oppo R17. Simu hii inakuja na sifa nzuri sana pamoja na muonekano mzuri sana.

Oppo R17 inakuja na RAM ya GB 8 ukubwa wa ndani wa GB 128 pamoja na fingerprint ambayo ipo juu ya kioo. Simu hii inaendeshwa na processor mpya ya Snapdragon 670 chipset yenye uwezo wa octa-core 2 GHz huku ikiwa na GPU ya Adreno 615.

Advertisement

Kwa mbele Simu hii inakuja na ukingo wa mbele maarufu kama top notch, lakini ukingo huo wa Oppo R17 ni mdogo sana tofauti na simu nyingine zenye ukingo huo. Kioo cha simu hii kina ukubwa wa inch 6.4 ambacho ni AMOLED screen chenye teknolojia ya Full HD+. Sifa nyingine za Oppo R17 ni kama zifuatazo.

Sifa za Oppo R17

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.4 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, 19:9 ratio (~394 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2 x 2.2 GHz Kryo 360 Gold na 6 x 1.7 GHz Kryo 360 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm Snapdragon 670 SoC Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 615
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 zote ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 8
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 25 yenye (f/2.0).
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 16 yenye uwezo wa (f/2.0) na nyingine ikiwa na Megapixel 5, huku zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500mAh battery yenye teknolojia ya (Fast battery charging) Fast battery charging: VOOC Flash Charge 5V/4A.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, microUSB 2.0, USB On-The-Go
    reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Stream Blue na Neon Purple .
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi wa Fingerprint kwenye kioo (Kwa Mbele).

Bei ya Oppo R17

Kwa upande wa bei, Simu mpya ya Oppo R17 itauzwa rasmi kuanzia August 18 na bei yake bado haijawekwa wazi ila inasemekana simu hiyo itauzwa kuanzia Euro 460, ambayo ni sawa na Tsh 1,195,000 bila kodi. Kumbuka ni muhimu kujua bei inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha pamoja na pale bei halisi itakapo Tangazwa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use