Kampuni ya Oppo ni moja kati ya kampuni zenye chimbuko lake nchini china na vilevile Oppo ni moja kati ya kampuni ambazo zinajulika sana kwa kuleta simu nzuri ambazo pia zinakuja kwa bei nafuu. Sasa baada ya kuzindua toleo la Oppo R17 Pro, Hivi karibuni kampuni hiyo imezindua simu yake nyingine ya Oppo K1 simu ambayo inakuja na sifa kabambe ukilinganisha na bei yake.
Simu hii mpya ya Oppo K1 inakuja na kioo cha inch 6.4 chenye resolution ya 2340×1080 pixel, simu hii pia inakuja na kioo kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED display, ambacho pia kinakuja na sehemu ya fingerprint ambayo iko juu ya kioo hicho.
Oppo K1 inakuja na kamera mbili za nyuma huku kamera moja ikiwa na Megapixel 16 na nyingine ikiwa na megapixel 2, kwa mbele simu hii inakuja na kamera moja ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 25 huku ikisaidiwa na mfumo wa AI kufanya simu hiyo kupiga picha kwa umakini zaidi, sifa nyingine za Oppo K1 ni kama zifuatazo.
Sifa za Oppo K1
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~402 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.0 GHz Kryo 260 & 4×1.8 GHz Kryo 260).
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 (14 nm) Chipset.
- Uwezo wa GPU – Adreno 512.
- Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa haina uwezo wa kuongezewa na memory card.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na RAM ya GB 6.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 25 yenye uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 16 MP, f/1.7, 1/2.8″, 1.12µm, PDAF na nyingine inakuja na Megapixel 5 yenye depth sensor. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS. microUSB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Blue na Red.
- Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
, Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. - Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Mbele Kwenye Kioo).
Bei ya Oppo R1
Kwa upande wa bei Oppo R1 kwa sasa inapatikana kwa kutoa oda nchini China kwa Yuan CNY 1,599 sawa na Tsh 529,000 bila kodi kwa toleo la Oppo R1 lenye RAM ya GB 4, Toleo lenye RAM ya GB 6 litauzwa kwa Yuan CNY 1,799 sawa na Tsh 595,000 bila kodi. Kumbuka kwa Tanzania bei inaweza kubadilika kutokana na kodi na viwango vya kubadilisha fedha.
Kkiukwel mko vizuri nimependa elimu ya biashara mnayotoa.lakin mm naomba msaada unijulishe simu nzuri ya oppo yenye uwezo mzuri wa betri, bei isiyozidi laki tatu na nusu,yenye uwezo mzur wa kamera pamoja na wake, na ukubwa wa ram pamoja na uwezo wa storage ya ndani ya cm.naomba nisaidie hilo ili nipate csimu nzurii