Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Hizi Hapa Sifa za Simu Mpya ya Oppo A3

Simu hii inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 128
Oppo A3 (2018) Oppo A3 (2018)

Kwa wapenzi wa simu za Oppo, leo kampuni hiyo imetangaza rasmi simu yake mpya ya Oppo A3 ambayo inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 128, processor ya Helio P60 chipset, ukingo wa juu maarufu kama Notch pamoja na kioo cha Full Display chenye inch 6.2 pamoja na aspect ratio ya 19:9.

Kwa mujibu wa tovuti ya Oppo, Simu hii mpya ya Oppo A3 inakuja na CPU yenye uwezo wa octa-core CPU yenye uwezo wa 2 GHz pamoja na GPU ya Mali-G72 MP3. RAM ya simu hii inakubwa wa GB 4 pamoja na sifa nyingine kama zifuatazo.

Advertisement

Sifa za Oppo A3

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia yaLTPS IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, 19:9 ratio (~405 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.0 GHz Cortex-A73 & 4×2.0 GHz Cortex-A53), Mediatek Helio P60 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP3
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 yenye uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye (f/2.2)
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 16 yenye (f/1.8), pamoja na teknolojia za phase detection autofocus, Geo-tagging, touch focus, face detection, HDR, panorama pamoja na flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Ion 3400 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Knight Black, Soybean Meal, Stardust Silver na Garnet Red.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint.

Kwa upande wa Bei simu hii inakuja ikiwa inauzwa kwa Yuan ya chini CNY2,099 sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 760,000. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa hapa Tanzania. Simu hii itanzaa kupatikana nchini China na kama tunavyojua kama itakuwa inapatikana nchini China basi ni kama vile Tanzania pia imefika…

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use