Hatimaye kampuni ya OnePlus imezindua simu zake mpya za OnePlus 7 Pro na OnePlus 7, simu hizi zinakuja na mtindo mpya kabisa huku zikiwa na maboresho makubwa sana hasa kwenye upande wa kioo.
Tukianza na simu mpya ya OnePlus 7 Pro, simu hii inakuja na kioo cha inch 6.67 ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ambayo OnePlus wanaita Fluid AMOLED. Kioo hicho kinakuja na uwezo wa resolution ya hadi QHD+ huku kikiwa na refresh rate ya hadi 90Hz, mbali na hayo kioo hicho pia kinakuja na uwezo wa kuonyesha video zenye mfumo wa rangi angavu za HDR10+.
Tukiachana na kioo OnePlus 7 Pro inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 16 ambayo inapatikana kwenye mota maalum ambayo huficha kabisa kamera hiyo na kufanya kamera hiyo kuto kuonekana na kuacha simu hiyo ikiwa na kioo kitupu. Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu zenye uwezo wa Megapixel 48, Megapixel 8 pamoja na Megapixel 16.
Simu hii inaendeshwa na processor yenye nguvu ya Snapdragon 855 chipset, ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 6, GB 8 au GB 12 pamoja na ukubwa wa ROM wa kati ya GB 128 au GB 256, bila kuwepo kwa sehemu ya kuongeza ukubwa huo kwa kutumia memory card. Sifa nyingine za OnePlus 7 Pro ni kama zifuatazo.
Sifa za OnePlus 7 Pro
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.67 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 3120 pixels, pamoja na uwiano wa 19.5:9 ratio (~516 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.80 GHz Kryo 485).
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm).
- Uwezo wa GPU – Adreno 640.
- Ukubwa wa Ndani – Zipo simu za aina mbili simu moja ikiwa na ROM ya GB 128 na nyingine GB 256, simu zote hazina sehemu ya kuweka memory card.
- Ukubwa wa RAM – Zipo simu za aina tatu, simu yenye RAM ya GB 6, GB 8 pamoja na GB 12
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 (Ikiwa kwenye Mota)
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/1.6, 1/2″, 0.8µm, Laser/PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/2.2, 13mm (ultrawide), na kamera ya tatu ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.4, 78mm (telephoto), 3x zoom, Laser/PDAF, OIS. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual-LED dual-tone.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, BDS, GALILEO, SBAS. USB 3.1 ya Type-C 1.0 reversible connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Mirror Grey, Almond na Nebula Blue.
- Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Mbele Chini ya Kioo).
Bei ya OnePlus 7 Pro
Kwa upande wa bei, inasemekana kuwa OnePlus pro itakuja ikiwa inauzwa kuanzia dollar za marekani $670 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Tanzania Tsh 1,545,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ROM wa GB 128. Kwa simu yenye RAM ya GB 8 na ROM ya GB 256 yenyewei itauzwa kwa dollar $700 ambayo ni sawa na Tsh 1,614,000 bila kodi. Vilevile Toleo la RAM ya GB 12 na ROM ya GB 256 itauzwa kwa dollar za marekani $750 ambayo ni sawa na Tsh 1,729,000 bila kodi. Kumbuka bei zote zinaweza kubadilika kwa Tanzania.
Tukija kwa upande wa OnePlus 7, simu hii yenyewe inakuja na kioo cha inch 6.41 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED ambacho pia kinakuja na uwezo wa resolution ya hadi 1080p+. Simu hii inakuja na ukingo wa mbele maarufu kama water drop notch, ukingo ambao unatumika kuhifadhi kamera ya Megapixel 16.
Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili zenye Megapixel 48 na Megapixel 5 ambazo zinasaidiwa na flash ya Dual-LED flash.
Mbali na kamera, OnePlus 7 inaendeshwa na Processor ya Snapdragon 855 chipset ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 8, pamoja na ukubwa wa ROM wa kati ya GB 128 na GB 256. Kama ilivyo OnePlus 7 Pro, simu hii pia haina sehemu ya kuweka Memory Card. Sifa nyingine za OnePlus 7 ni kama zifuatazo.
Sifa za OnePlus 7
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.41 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, pamoja na uwiano wa 19.5:9 ratio (~402 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.80 GHz Kryo 485).
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm).
- Uwezo wa GPU – Adreno 640.
- Ukubwa wa Ndani – Zipo simu za aina mbili simu moja ikiwa na ROM ya GB 128 na nyingine GB 256, simu zote hazina sehemu ya kuweka memory card.
- Ukubwa wa RAM – Zipo simu za aina mbili, simu yenye RAM ya GB 6 na GB 8
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 (Ikiwa kwenye Mota)
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/1.6, 1/2″, 0.8µm, Laser/PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.4, 1.12µm. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual-LED dual-tone.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3700 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, BDS, GALILEO, SBAS. USB 3.1 ya Type-C 1.0 reversible connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Mirror Gray, Red.
- Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Mbele Chini ya Kioo).
Bei ya OnePlus 7
Kwa mujibu wa OnePlus, bei ya OnePlus 7 bado hakuna taarifa kuhusu bei ya simu hii. Kujua zaidi kuhusu bei ya simu hii hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha pindi bei hiyo itakapo Tangazwa.