Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kutana na Nubia Alpha Simu ya Kuvaa Mkononi Kama Saa

Hii hapa saa yenye kioo chenye inch 4.0
Video thumbnail for youtube video 0kvsd6boiw4 Video thumbnail for youtube video 0kvsd6boiw4

Mkutano wa MWC 2019 umeingia siku ya tatu na leo ni zamu ya kampuni ya Nubia. Kampuni ya Nubia ambayo ni sehemu ya kampuni ya ZTE, hapo jana ilitangaza simu yake mpya ya Nubia Alpha ambayo ina muundo wa saa lakini pia ikiwa na kioo kikubwa chenye inch 4.0.

Simu hiyo mpya ya Nubia Alpha inafanya kazi kama smartwatch lakini pia ukinyoosha mikanda yake, utapata kioo hicho cha inch 4.0 chenye uwezo wa kukupa uwezo wa kutumia saa hiyo kama smartphone ya kawaida.

Advertisement

nubia Alpha

Simu hii ambayo pia ni saa ina kuja na processor yenye nguvu ya Snapdragon Wear 2100 chipset ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 1 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 8. Nubia Alpha inatumia mfumo wa Android Wear 2.1, mfumo ambao ni maalumu kwa ajili ya saa janja au Smartwatch.

Hata hivyo unaweza kutumia Nubia Alpha kama simu kwa kuunganisha laini ya eSIM moja kwa moja kupitia mtandao wa simu unaotaka kutumia, Kwani saa hii ambayo pia ni simu haina sehemu ya kuweka laini hivyo ni lazima kutumia mfumo huo wa laini za kidigitali kama unataka kutumia saa hiyo kama simu ya kuweza kutuma ujumbe mfupi (SMS), pamoja na kupiga na kupokea simu.

Nubia Alpha pia inakuja na kamera ya Megapixel 5 ambayo iko mbele ya saa hiyo. Unaweza kutumia kamera hiyo kupiga picha kuchukua video pamoja na kupiga simu za Video (Video Call). Kufanya mambo yote hayo Nubia Alpha inaendeshwa na battery ya 500mAh yenye uwezo wa kufanya saa hiyo kudumu na chaji kwa muda wa siku mbili kulingana na matumizi yako.

Nubia Alpha inapatikana kwa matoleo mawili, toleo moja linakuja na mtandao wa eSIM na toleo lingine linakuja na Bluetooth ambapo unaweza kuitumia na simu yako. Saa hii inapatikana kwa euro €450 ambayo ni sawa na Tsh 1,199,000. Hata hivyo kwa toleo lenye eSIM litauzwa kwa €650 ambayo ni sawa na Tsh 1,731,000 bila kodi.

https://www.tanzaniatech.one/mwc-2019/

1 comments
  1. Asante sana kwa Ujumbe huo mzuri!!!!
    Nina shida moja naomba msaaada wako tafadhali..nina smartwatch aina ya W87, nimeshindwa kuifanya laini kusoma ndani ya smartwatch hii, kwani nikipachika laini inaandika INVALID SIM.

    Natumai utanisaidia kwa hilo. Asante

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use