Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya ya Nokia X71

Zifahamu hapa kwa undani hizi hapa sifa na bei ya Nokia X71
Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya ya Nokia X71 Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya ya Nokia X71

Habari njema kwa wapenzi wa simu za Nokia, baada ya kampuni ya Nokia kuzindua simu mpya ya Nokia 9 Pureview hivi leo kampuni hiyo imerudi tena na simu mpya ya Nokia X71. Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, simu hii inaitwa X71 kwa upande wa China lakini inasemekana itakuja kwenye nchi nyingine kote duniani ikiwa inaitwa Nokia 8.1 Plus.

Mbali na hayo vilevile simu hii mpya ya Nokia X71 au Nokia 8.1 Plus ndio simu ya kwanza kabisa kuja na mfumo wa kamera kama za simu za Galaxy S10 ambapo sehemu ya kamera ya mbele inakuwa juu ya kioo.

Advertisement

Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya ya Nokia X71

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, simu hii inakuja na kioo cha inch 6.39 chenye resolution ya 1080 x 2316 pixels. Vile vile kioo hicho kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD pamoja na FHD+. Kamera ya mbele ya simu hii inakuja na uwezo wa Megapixel 16, huku ikiwa juu ya kioo na kufanya simu hii kuwa na kioo kikubwa.

Mbali na kamera ya mbele, Nokia X71 inakuja na kamera tatu kwa nyuma huku kamera moja ikiwa na Megapixel 48, na nyingine MP 8 na kamera ya mwisho inakuja na uwezo wa megapixel 5. Kamera zote hizi zinauwezo wa kuchukua video za 4K pamoja na picha zinazopigwa kwenye mwanga hafifu.

Mbali na kamera, Nokia X71 inaendeshwa na processor ya Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 128. Ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa memory card hadi ya GB 256, Sifa nyingine za Nokia X71 ni kama zifuatazo.

Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya ya Nokia X71

Sifa za Nokia X71

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.39 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2316 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie), yenye Android One
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Kryo 260 & 4×1.8 GHz Kryo 260).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 (14 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 512.
  • Ukubwa wa Ndani (ROM) – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye f/2.0.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/1.8, 1/2″, 0.8µm, PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 8 ambayo ni 13mm (ultrawide), kamera ya mwisho ina Megapixel 5 ambayo ni f/2.4, depth sensor. Kamera zote zikiwa zinasadiwa na Zeiss optics, dual-LED dual-tone flash, panorama, na HDR.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 18W.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa moja ya Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Nokia X71

Kwa upande wa bei ya Nokia X71, simu hii inasemekana kupatikana kwa nchini Taiwan na itakuwa inauzwa kwa Dollar ya Taiwan TWD 11,900 ambayo ni sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 894,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kodi na viwango vya kubadilisha fedha.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use