Kampuni ya Nokia hivi leo imetangaza simu mpya ya bei rahisi ya Nokia C2 (2020), simu hii inakuja ikiwa ni simu inayotumia mfumo wa Android 9.0 Pie (Go edition), mfumo ambao ni maalum kwaajili ya simu zenye RAM chini ya GB 1.
Simu hii mpya ya Nokia C2 (2020), inakuja na kioo chenye ukubwa wa inch 5.7 kioo ambacho kimetengezwa kwa teknolojia ya IPS LCD ambacho pia kinakuja na resolution ya hadi pixel 720 kwa 1440.
Kwa upande wa kamera, Nokia C2 (2020) inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 5 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za resolution ya hadi 720p@30fps. Kamera hiyo pia inakuja na sehemu ya Flash ambayo husaidia kupiga picha za selfie wakati wa usiku.
Kwa nyuma Nokia C2 (2020) inakuja na kamera moja ambayo nayo pia inakuja na uwezo wa Megapixel 5, huku ikiwa inasaidiwa na Flash ya LED pamoja na teknolojia ya HDR. Kamera hii pia ina uwezo wa kuchukua video za hadi 720p@30fps. Sifa nyingine za Nokia C2 ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Nokia C2
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.57 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1440 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 Pie (Go edition)
- Uwezo wa Processor – Quad-core 1.4 GHz.
- Aina ya Processor (Chipset) – Unisoc (28nm)
- Ukubwa wa Ndani – GB 16
- Ukubwa wa RAM – GB 1.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 5. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 2800 mAh.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE
na GPS ya A-GPS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go. - Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Cyan na, Black.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G
- Ulinzi – Haina Fingerprint.
Bei ya Nokia C2
Nokia C2 (2020) inategemea kupatikana hivi karibuni, lakini hadi sasa wakati habari hii inachapishwa kampuni ya Nokia kupitia HMD Global bado ilikuwa haijatangaza bei ya simu hii. Kama unataka kujua bei ya simu hii hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.